Jumanne, 20 Mei 2014

Picha 18 za kwanza za msiba wa Adam Kuambiana Leaders Kinondoni kutoka kwa millardayo


Home » Ent. » Picha 18 za kwanza za msiba wa Adam Kuambiana Leaders Kinondoni



Picha za kwanza za msiba wa Adam Kuambiana Leaders Kinondoni kutoka kwa millardayo


3kuambianaKwa sasa kutoka hapa Leaders ni watu mbalimbali wanatoa heshima zao za mwisho wakiwemo waigizaji mbalimbali ambao marehemu Adam Kuambiana aliwahi kufanya nao kazi na wengine ambao hawakuwahi kufanya nae kazi,kwa mujibu wa ratiba iliyotangazwa mazishi yanategemewa kufanyika saa 9 kwenye makaburi ya Kinondoni.
Miongoni mwa watu waliokuwa na simanzi zaidi mpaka wakashindwa kuongea ni Jb hakumalizia kuongea akawa anataka kudondoka chini,endelea kufatilia millardayo.com kwa taarifa zaidi.
1kuambiana
9kuambiana
18kuambiana
17kuambiana
16kuambiana
15kuambiana
14kuambiana
13kuambiana
12kuambiana
11kuambiana
10kuambiana
8kuambiana
7kuambiana
6kuambiana
5kuambiana
4kuambiana

1kuambianaUngana na mimi kwenye twitter kwa kubonyeza HAPA, pia FACEBOOK & INSTA ili niwe nakutumia kila taarifa inayonifikia, picha nyingine nitakuwekea hapa baadae
 source millardayo.com

Dimond Platinumz hakamatiki kwa wiki ya pili sasa kwenye mashindano ...................KORA

Mtanzania: Mishezo na Burudani:  Zikiwa zimebakia siku chache kabla ya mashindano yanayowahusisha wasanii wakali wote ulimwengunina  kufikia tamati na washindi kupatikan...

Jumatano, 5 Machi 2014

Ajira mpya za wlimu 2013/2014

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA AJIRA KWA WALIMU WAPYA MWAKA 2013/14

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK HAPA CHINI

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA AJIRA KWA WALIMU WAPYA MWAKA 2013/14

Jumla ya Walimu wapya 36,021 ambao wamehitimu mwaka 2013 kutoka vyuo mbalimbali hapa nchini wataajiriwa rasmi na Mamlaka za Serikali za Mitaa (Halmashauri) ifikapo tarehe 01 Aprili 2014. Kati ya idadi hiyo walimu wa ngazi ya Cheti (Daraja III A) ambao hufundisha katika shule za Msingi ni 17,928 na walimu wa shule za sekondari ni 18,093 (wakiwemo 5,416 wa Stashahada na 12,677 wenye shahada).

Orodha rasmi ya walimu wapya ikionesha Halmashauri mbalimbali walikopangwa itatangazwa kwenye tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI (www.pmoralg.go.tz) na ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (www.moe.go.tz) ifikapo tarehe 15 Machi, 2014.

Walimu wote wapya wanatakiwa kuripoti bila kukosa kwenye Halmashauri walikopangiwa ifikapo tarehe 01 Aprili, 2014 ili waanze kazi mara moja.

Inasisitizwa kwamba walimu waripoti tarehe hiyo ili taarifa zao za kiutumishi zifanyiwe kazi na Waajiri wao yaani Wakurugenzi ili kuwawezesha kupata mshahara mwezi Aprili 2014 na hivyo kuepuka ulimbikizaji wa mshahara kwa watumishi wapya wanaoanza ajira.

Mwalimu yoyote ambaye ataripoti baada ya tarehe 10 Aprili, 2014 bila sababu za msingi zinazokubalika kiutumishi atakuwa amepoteza nafasi hiyo.

Ikumbukwe kwamba Upangaji wa Walimu wapya kwenye Halmashauri umezingatia uwepo wa mahitaji ya walimu. Vile vile, fedha za kujikimu kwa muda wa siku saba na nauli ambazo zitalipwa kwa kila mwalimu atakayeripoti kulingana na viwango vilivyowekwa na Serikali zimetumwa kwenye Halmashauri walikopangwa walimu hao. Hivyo, kila mwalimu anatakiwa kwenda kuripoti katika Halmashauri alikopangwa.

Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI haitafanya mabadiliko yoyote ya vituo vya kufanya kazi walimu wapya isipokuwa kwa utaratibu wa kawaida wa uhamisho baada ya mwalimu kutimiza vigezo na masharti ya uhamisho.

Ni vema ifahamike kuwa ajira zinazotangazwa ni za walimu wapya. Walimu ambao tayari ni watumishi umma waliokuwa vyuoni kwa ajili ya kujiendeleza kielimu na hivi sasa wamehitimu mafunzo yao, wanatakiwa kurudi kwa waajiri wao na kuendelea na kazi.

IMETOLEWA NA
JUMANNE A. SAGINI
KATIBU MKUU
OFISI YA WAZIRI MKUU - TAMISEMI

Jumatatu, 3 Machi 2014

WIZARA YA ELIMU ELIMU TANZANIA YAZIDI KUBORONGA



                                                   
    Wizara ya elimu ya Tanzania imeendelea kufanya hovyo katika maamuzi na utendaji wa           mambo   yake.
 Halii hii inajidhihirisha kwa kuwapa walimu tarajali (walimu waliopo vyuo vya Serikali,wa ngazi ya cheti na Stashahada) pesa  ya kujikimu  wakiwa  katika mazoezi ya vitendo  (field) kiasi cha  shilingi  4500 (elfu mianne na miatano tu ) .
Hii sio bahati mbaya kwa sababu utaratibu huo wakuwapa wanavyuo hao wanaosomea ualimu ulianza mwaka jana na walilipwa pia 4500 wakiwaahidi kuwa kwa  kuwa ni mfumo mpya hivyo mwaka utakaofuatia yaani mwaka huu wa 2014 wange waongeza pesa lakini hali imebakia kuwa hivyo hivyo.

Utaratimu wa miaka yanyuma 2012 kurudi nyuma ilikuwa wanachuo walio katika vyuo vya ualimu vya serikali  wanapoenda kwenye mazoezi ya vitendo walikuwa wakipewa chakula na fedha kiasi za kujikimu wanapo kuwa huko lakini kwanzia mwaka jana wamekuwa wakipewa shilingi 4500 tu.
 Katika hali ya kawaida tujiulize hiyo pesa inatosha nini ikiwa wanavyuo waliopo vyuo vikuu huwa wanalipwa shilingi 7500 kwa siku kama pesa yao ya kula wakiwa chuoni na wanapo enda (field) kwenye mazoezi ya vitendo huwa walipwa (10000) elfu kumi .

 Ukiangalia mazingira ya hawa walimu wavyuo vikuu na wa stashahada hata Cheti  wote wanaenda Field maeneo yale yale na maanisha shule zile zile na kama changamoto ni sawa tu sasa kwanini kuwe na tofauti  za posho za kujikimu wanapo kuwa huko huu ni udhaifu wa hali ya juu Wizara inabidi iji sahihishe katika upangaji wake wa mambo.Na hiyo pesa ya shilingi 4500 haitoshi kwa maisha ya sasa mtasababisha wadogo zetu wakike kujiuza huko na kuvunja ndoa za watu.
Kama haiwezekani utaratibu wa zamani ukirudishwa ni vizuri pia.

Maana ikiwa watu wanagomea laki tatu Bungeni kwenye Bunge La katitiba  hawa wanaokubali 4500 unadhani vichwani mwao wafikiria nini  kama sio ni mgomo baridi?.
   
Nchi yenye utawala Bora haiwezi kuwandaa Bora walimu na sio Walimu Bora.
                              Wakikuuliza kaandaa nani waambie korumba Mtanzania

Ijumaa, 28 Februari 2014

Madudu (5) matano ya Wizara ya Elimu yaliyo weka historia Duniani mwaka 2013/2014



      Madudu (5) matano  ya  Wizara ya Elimu yaliyo weka historia Duniani mwaka 2013/2014
   Mwaka 2013 na 2014  umekuwa ni mwaka wenye maajabu ya madudu ambayo hayajawahi kutokea katika sekta ya elimu Tanzania.Maajabu hayo nikama  yafuatayo
1.MATOKEO
Kutangaza matokeo ya kidato channe ya mwaka 2013/2014 kwa viwango vipya vya madaraja ya ufaulu yaliyo pingwa sana na watanzania na Wabunge bungeni  Kabla yakutumika kwa kuwa  viwango hivyo ambavyo havileti maendeleo katika sekta ya elimu zaidi ya kudhorotesha sekta ya elimu Tanzania.
2.Ajira
27/2/2014 Wizara kupitia gazeti la Tanzania Daima ilitangaza kuwa imewaajiri walimu 360000 bila kutoa majina ya walimu hao na ambao wameajiriwa kitu ambacho hakikuwahi kutokea tangu Wizara hiyo ilipoanzishwa.
3.Mazoezi ya Vitendo
Mazoezi ya vitendo kwa walimu Tarajari waliopo vyuoni haijawahi kutokea wakachelewa kwenda kwenye mazoezi hayo ya vitendo kama ilivo sasa mwezi wapili unaisha bado tu wapo vyuoni bila sababu za maana.
4.Kusoma nakuandika
 Haijawahi kusikika Duniani kote kuwa kuna wanafunzi wanaomaliza shule ya msingi na kufanya mitihani kisha kufaulukuendelea  na wanapoenda shule ya upili yaani secondari washindwe kusoma na kuandika lakini kwa Tanzania hilo lime tokea na limesha zoeleka na kuwa kama kitu cha kawaida tu.
5.Tovuti
Mwisho kabisa ukiingia kwenye tovuti yao ya wizara ya Elimu kunasehemu ya kutoa maoni ya Yule anaetazama tovuti hiyo watu wengi wamekuwa wakitoa maoni kuwa mfumo ni mbovu kwa zaidi ya  48% Kitu ambacho ni ajabu kutokea kwa nchi nyingine pia tovuti hiyo haivutii kila siku vitu nivilevile.
             INCHI YENYE UTAWALA BORA HAIWEZI KUWA NA ELIMU MBOVU

Ijumaa, 21 Februari 2014

Matokeo ya kidato cha nne 2013 Zero bado ni Tatizo sugu

NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2013

Wanafunzi 74,324 sawa na asilimia 21.09 wamefaulu katika madaraja ya I -III.

Jumla ya watahiniwa 427,679 waliandikishwa kufanya mtihani ila waliofanikiwa kufanya mtihani ni watahiniwa 404,083.
Jumla ya watahiniwa laki 235,227 sawa na asilimia 58.25 ya waliofanya mtihani wamefaulu.
Wasichana waliofaulu ni laki 106,792 na wavulana waliofaulu ni laki 128,435. 
Wanafunzi 74,324 sawa na asilimia 21.09 wamefaulu katika madaraja ya I -III.
Wavulana waliopata daraja la kwanza (division one) ni 5,030 na wasichana ni 2,549.
Wavulana waliopata daraja la tatu (Division 3) ni 27,904 na wasichana ni 17,113. 
Jumla ya wanafunzi waliopata daraja la 4 (division 4) ni laki 126,828, wasichana wakiwa 62,841 na wavulana 63,987.
Jumla ya wanafunzi laki 151,187 wamepata ’0′ (division ziro) . Wasichana ni 72,237 na wavulana ni 78,950. 
Shule 10 zilizoongoza ni St.Francis Girls, Marian Boys, Feza Girls, Precious Blood, Canossa, Marian Girls, Abbey
Shule kumi zilizoongoza: Anwarite Girls, Rosmini, na DonBosco Seminary
Zilizofanya vibaya: Singisa, Hurui, Barabarani, Nandanga, Vihokoli, Chongoleani, Likawage, Gwandi, Rungwa, Uchindile

ACSEE 2013 EXAMINATION RESULTS ENQUIRIES

KWA KUANGALIA MATOKEO BOFYA HAPA 
Chanzo: kingo tanzania

Jumapili, 16 Februari 2014

Sauti ya Vijana BUSOKELO watoa zawadi kwa washindi wao

SAUTI YA VIJANA BUSOKELO WAFANYA YAO!!!!! Mnamo tarehe 2/2/2014 walitoa tangazo katika ukurasa wa sauti ya vijana busokelo Facebook kuwa...