Jumamosi, 30 Novemba 2013

Mwenye kiti wa Chadema Mkoa Wa Lindi Ajiuzulu sababu ya Zitto

Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Lindi ajiuzulu. Adai Kamati Kuu ya CHADEMA imefanya maamuzi ya kijuha!

Hii chini ni taarifa yake aliyoisambaza kwa vyombo vya habari:


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI YA NDUGU ALLY O. CHITANDA

NDG: WANA HABARI:
Kwanza kabisa ninawashukuru kwa kuitika wito wangu.

Jina langu naitwa ALLY OMARY CHITANDA, nimejiunga CHADEMA mwaka 2003 nikitokea NCCR –MAGEUZI.

Nyadhifa nilizowahi kuzishika na kukitumikia Chama ni:-

Kuanzia mwaka 2004- Mjumbe wa Baraza kuu Taifa nikiwakilisha vijana Bara niliendelea kuaminiwa na Chama na kupewa kazi nyingine za kukitumikia Chama, nimewahi kuwa Afisa wa Vijana Makao Makuu, Afisa wa sheria na Haki za binadamu Makao Makuu, Katibu wa Kamati ya muda ya Baraza la Vijana Taifa (BAVICHA) kwa sasa ni Mjumbe wa Mkutano Taifa nawakilisha Nachingwea, Mwenyekiti wa Mkoa wa Lindi tangu tarehe 26/05/2013.Pia ni Afisa Mwandamizi Ofisi ya Katibu Mkuu Makao makuu Dsm.

vile vile kwa kipindi kirefu sasa nimekuwa nikifanya shuhuli ya uandishi wa kumbukumbu za sekretarieti ya chama kama KATIBU WA SEKRETARIETI YA KAMATI KUU.
Hivyo sasa, pamoja na mambo mengine yapo masuala nyeti na muhimu ninayoyafahamu na ikibidi kuwaarifu watanzania kwa njia mbali mbali pindi itakaponihitaji kufanya hivyo.

Ndugu zangu wanahabari, nimewaita ili kupitia nyinyi niwaambie Watanzania wenzaqngu juu ya hali ya kisiasa ilivyo hasa ndani ya Chama chetu. Itakumbukwa kuwa tarehe 20-21/11/2013 Kamati kuu ya Chama ilikaa pamoja na mambo mengine ilifanya maazimio ya kuwavua nafasi za Uongozi ndani ya Chama alikuwa Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara Mhe. ZITTO KABWE na Mjumbe wa Kamati kuu wa kuchaguliwa Mhe. Dr. FITILA MKUMBO, kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kwa sababu:-

(a) Mhe. ZITTO KABWE (Mb) alishiriki kusaidia Wabunge watatu wa CCM kupita bila kupingwa kenye Majimbo yao ya Uchaguzi 2010.

(b) Kuandaa mkakati waliouita mabadiliko ya Chama 2013. Mkakati uliolenga kumuwezesha Mhe. Zitto kushinda nafasi ya Uenyekiti wa Chama Taifa endapo angekubali kugombea.

(c) Mhe. Zitto alishindwa kutimiza majukumu yake ndani ya Chama kwa kutoshiriki pamoja na Viongozi wenzake kwenye matukio makubwa yaliyokikumba Chama kama:-
(i) Maandamano ya Arusha.
(ii) Operesheni zilzofanyika Morogoro na Iringa nk.

MAAMUZI MENGINE YA UBORESHAJI WA MAKAO:
Ni kweli kuwa pamoja na mambo mengine Baraza kuu la Chama iliridhia pendekezo lililetwa kwake na Kamati Kuu kuhusu jambo hili.Na katika utekelezaji wake Kamati Kuu ya juzi iliridhia kuwa, uteuzi wa Wakurugenzi watano ambao ni:-
1. Mkurugenzi wa Oganaizesheni Mhe. Singo Kigaila Benson.
2. Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mahusiano ya ndani Mhe. John Mnyika (Mb).
3. Mkurugenzi wa Fedha na uwekezaji Mhe. Anthony Komu.
4. Mkurugenzi wa Bunge na Halmashuri Mhe. John Mrema.
5. Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama Mhe. Wilfred Lwakatale.

Uteuzi huu hauonyeshi sura ya Kitaifa Wakurugenzi wote watano ni Wakristo kanakwamba CHADEMA hakuna Waislamu wenye uwezo wa kushika nafasi hizo.

Lakini pia hauzingatii mgawanyo wa kijamii kwa kuwa kati ya kurugenzi hizo sita wakurugenzi wanne kati yao wanatokea mkoa mmoja wa kilimanjaro

Na uteuzi huu unakwenda sambamba na kuboresha maslahi yao kwa kuongeza posho, -kutoka Tshs. 800,000/= za awali na sasa itakuwa ni kuanzia Tshs. 1,500,000-2,500,000/= kwa Mkurugenzi na kutoka Tshs. 6,800,000/= kwa Afisa Mwandamizi na sasa ni Tshs.1,000,000-1,500,000/=.

Pamoja na kwamba uboreshaji uliridhiwa, lakini katika mpango ulioridhiwa na Baraza kuu ni pamoja na kulipa Posho kwa Makatibu wa Wilaya na Mikoa. Hawa ndio watendaji muhimu katika Ujenzi na Uhai wa Taasisi hii lakini, hawakuangaliwa wala kuguswa badala yake wanatakiwa kujitolea tu kwa hali na mali.

Mimi kama nilivyotangulia kusema hapo awali, kuwa niko kwa kwa miaka 10 sasa na nimeshiriki kwa kiasi kikubwa katika Ujenzi wa Chama hiki.Sioni sababu ya kutoharakisha kulipa posho ya Mkatibu wa Wilya na Mikoa pamoja na watendaji wengine na badala yake tunaharakisha kujilipa posho nono sisi watendaji wa Makao Makuu, wakati hawa wa ngazi za chini wanamaeneo makubwa ya Kiutendaji na wanafanya kazi katika mazingira magumu kwa kujitolea hata Ofisi zao wanajitolea wenyewe.

MAAMUZI YA KAMATI KUU
Ningependa kuwaambia wanachadema na watanzania kwa ujumla, maamuzi haya ya kamati kuu ya kuwavua uongozi zitto kabwe na dkt mkumbo ni maamuzi ya kijuha na yanayowafanya watanzania sasa waangalie mara mbili mbili kama hawa watu wapo makini na huo ukombozi wanaousema.

Tumekuwa tukiweka mikakati mbali mbali ya ushindi ili chama kishinde, kwa mfano, kabla hata ya kifo cha aliyekuwa mbunge wa arumeru mashariki, wakati tu ilipobainika anaugua, chama kiliandaa mkakati wa kushinda ubunge wa jimbo hilo na uchaguzi uliporudiwa mkakati ule ulitumika na kushinda.

Nikiwa mtendaji wa ofisi ya katibu mkuu, nimeshiriki pamoja na zitto kabwe na dkt Slaa kupanga mikakati mbali mbali mizuri na mibaya kwa nchi, lakini hatukuwahi kuitwa wasaliti, wahaini wala sina lolote baya. Ni fedheha leo mimi kuwa sehemu ya watu wanaomuita zitto kabwe ni msaliti. Siwezi kuendelea na ujinga huu na sipo tayari tena.

Si dhambi kumuhukumu mtu kwa kuwa anapanga mipango ya kukushinda kwenye uchaguzi, dawa ya mpinzani wako ni kumkabili.

Naomba nikiri kwamba nikiwa katibu wa sekretarieti tumekuwa tukilazimishwa mara kadhaa kuwashawishi wajumbe wengi kutowaunga mkono watu wenye misimamo thabiti ndani ya chama na badala yake tumekuwa tukitumia rasilimali za chama kuwajenga wajumbe ndio.

Kwa mfano hivi sasa tunapozungumza, wakati katibu mkuu wa chama anasema mjadala wa zitto kabwe umefungwa rasmi, amewaagiza wakurugenzi wa chama kuzunguza nchi nzima kusambaza waraka waliouandaa ukimchafua zitto. Hii si sawa hata kidogo, si vema kutumia rasilimali za chama kuwanufaisha watu binafsi kutimiza matakwa yao ya kisiasa.

Nafsi yangu haipo tayari kuendelea kuwa sehemu ya upotoshaji dhidi ya watanzania wenzangu.

Nafsi yangu inanikataza kabisa kuendelea kufumbia macho maovu yanayoendelezwa na chama changu.

Nafsi yangu imechoka kuendelea kushuhudia ubaguzi wa kidini na kikabila unaofanywa wazi wazi na viongozi wa chama changu.

Nafsi yangu imekataa sasa, haipo tayari tena kuwa kuwadi wa kuwahadaa Watanzania kuyafikia matarajio tunayowapa ambayo kamwe hayafikiki.

Kwa kuwa siamini kwamba kuvuliwa nyadhifa kwa zitto kabwe na dkt kitila mkumbo ni kwa sababu ya waraka wa ushindi, bali ninaamini kuvuliwa kwao ni kutokana na hofu ya uchaguzi, ubaguzi wa kikabila na kikanda.

Hivyo basi, nikiwa na akili timamu kabisa, leo tarehe 30.11.2013 nimeamua kujivua nyadhifa zangu zote nilizokuwa nazo ndani ya chama.

Sioni tena sababu ya kuendelea kuwa MwanaCHADEMA, sioni tena sababu ya kuwa mwenyekiti wa CHADEMA MKOA WA LINDI, sioni tena sababu ya kuwa KATIBU WA SEKRETARIETI YA KAMATI KUU.

Kwa kuwa vipaumbele vya chadema ni kukijenga chama mikoa ya kaskazini. Basi sisi wananchi wa mkoa wa lindi tunawatakia kila la heri, na kwamba waendelee kukijenga chama chao huko huko waliko.

Nashukuru wote ambao nilifanya nao kazi pamoja katika kutekeleza majukumu yangu.

Ahsante Sana

A.O. CHITANDA

0753418510

MWENYEKITI CHADEMA MKOA LINDI
MJUMBE BARAZA KUU TAIFA
KATIBU OFISI YA KATIBU MKUU- SEKRETARIETI

Mtazamo wa Msudi Kipanya juu ya mwenendo wa chama cha Chadema

Ijumaa, 29 Novemba 2013

Tazama picha na kilicho andikwa leo na Korumba victor moshi Leo ambayo ni siku yake ya kuzaliwa

Mimi ni mtoto wa 3 kuzaliwa katika familia ya mzee Antoy mwenyeji wa Marangu Kilimanjaro.Nilizaliwa miaka 20 iliyopita Marangu Samanga
namshukuru Mungu Baba,Mwana na Roho mtakatifu kwa uzima na neema nayoipata ya kuendelea kuishi hadi hivi sasa.
Wapili ni Mama yangu mzazi yeye ndo kila kitu kwangu kanilea na anaendelea kunilea vizuri maana kwake mimi kama motto siwezi kukua.Siwezi kurudisha hata robo ya fadhil zake kwangu ila ahadi yangu kwake nitampenda wakati wote maana kaweza kunilea kwa kadri mungu alivo muwezesha baada ya kifo cha marehemu Baba yangu mungu pia amlaze mahali pema.
3. Kaka yangu Essau Ngobei Yeye huyu Anamchango mkubwa pia katika maisha yangu nathubutu kusema huyu kwangu ndio SOMO WANGU (Rol model) yeye kwangu ni mwalimu,yeye kwangu ni boss kamwe siwezi nika msamsahu katika mafanikio yangu.
4. RECHAL MONGI huyu pia ni dada yangu yeye ni mshauri wangu namba moja katika maishay yangu amekuwa akinitia moyo napokata tama na kunisaidi napokuwa na shida nampenda sana nay eye pia analijua hilo
5.Kampuni nazofanyia kazi SWIVEL MARKETING NA VODA COM Naamani kufanya kazi na nyinyi na muda wote nimekuwa mwaminifu kwa majukumu yangu nayoyasimamia ili nisiangushe utendaji wa kampun i kwa ujumla nyinyipia mchango wenu nauthamini
6.Chuo cha JERUSALEM TRAINING COLLEGE Kilichopo Dodoma mimi nikiwa kama mkurugenzi mtendaji wa chuo hichi nashukuru na natambua saport ya Boss wangu kwangu katika kutimiza malengo yangu namalengo ya chuo pia
7.Mbonachi Matola,Jr Stories, Brina Baibey, Bakamaza sospeter, Anord Kasomo, Job mwalukasa,sumi Odilo,Aleleuya Maumbi,Aleni Maluli,Neema lizer,Angel Shayo,Abdul Senganya,Carolina Mohamed,Shukuru Gerald,Mud Gora,Method Nyunza,Erasto Marwa,Sindano Masanja,Elia Mlowezi,Daudi kipasiwinga,Regnald Daniel
8. Kwa wote ambao nime sahau kuwaandika haina maana kwamba umuhimu wenu si utambui nashukurun pia kwa saport yenu kwangu
Mimi ni MTANZANI NA NAJIVUNIA KUWA HIVO NA NDO MANA NIMEVAA MADE IN TANZANIA
Tudumishe amani one love


Alhamisi, 28 Novemba 2013

Katuni pendwa ya CHADEMA

WOLPER NA WEMA HAWANA TOFAUTI


WOLPER:ALIKIBA NDO ALINIFUNZA MAPENZI
♠ Posted by lucky junior at 20:21
Na Sifael Paul
MOYO huhifadhi mengi mazito hasa ya kuumiza! Staa mkubwa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe amejikuta akimwaga machozi wakati akianika siri tano nzito kuhusu mapenzi katika mahojiano (exclusive interview) na Amani kwa takriban saa mbili.
Wolper akifunguka ndani ya Ofisi za Global Publishers, Bamaga-Mwenge jijini Dar.
Katika ‘intavyu’ hiyo iliyofanyika Jumatatu iliyopita kwenye Ofisi za Global Publishers, Bamaga-Mwenge jijini Dar kuanzia saa 8:44 alasiri hadi saa 10:44 jioni, Wolper alifunguka vitu vingi.
KISA/MKASA
Akizungumza kwa masikitiko, uchungu na majuto, Wolper alisema hawezi kumsahau mwanaume huyo ambaye ni Abdallah Mtoro ‘Dallas’ kwa namna alivyomwingia kijanja na kutaka kumvunjia heshima aliyoijenga karibia miaka kumi nyuma.
Wolper akijibu maswali ya Global.
ALIANZIA WAPI NA DALLAS?
“Siku ya kwanza Dallas alinipigia simu na kuniambia aliniona Magomeni (Dar). Naikumbuka sana siku hiyo, ilikuwa baada ya mizunguko yangu, mwanzoni sikupokea simu yake kwa sababu ilikuwa namba ngeni kwangu.
“Nilimsikiliza sana. Jamani yule mwanaume anaongea kwa ushawishi wa hali ya juu mno. Nilishangaa aliponieleza kila kitu kuhusu familia yangu na nyumbani kwetu. Kumbe tayari alishaunda urafiki na baba yangu (mzee Massawe).
“Mwanzoni nilidhani ni tapeli. Nikamkatia simu. Akaendelea kunipigia na nilipoona imekuwa kero kubwa nilipokea. Ili kuthibitisha anawajua wazazi wangu, alinitajia namba zao za simu ambazo ni za kweli.
“Pamoja na hilo nilimfanyia nyodo, si unajua mtoto wa kike? Lakini aliniongelesha kwa upole hadi nikapunguza nyodo zangu.
“Aliniuliza nataka anifungulie biashara gani. Nikamwambia biashara ya nguo. Akaniuliza nataka mtaji kiasi gani. nikamwambia dola laki moja kwa sababu nilikuwa sitaki fremu moja, nilitaka nyumba nzima. Akaniambia hakuna tatizo.
“Pia aliniuliza naishi wapi? Nikamwambia Sinza (Dar) alionesha dharau kwenye simu akaniambia atanihamishia Mbezi Beach.
“Aliniuliza natembelea gari gani? Nikamwambia Toyota Noah. Akaniambia ningependa aninunulie gari gani? Nikamjibu Toyota Discovery lakini yeye akasema ataninunulia Toyota Harrier.
“Kweli baada ya siku mbili-tatu nililetewa Toyota Harrier nyeusi nyumbani. Niliogopa isijekuwa mtego nikaingia kwenye matatizo hivyo nilimzungusha mtu aliyeniletea hadi Sinza-Mori nikamwambia apaki kwenye kituo cha teksi, nikaenda na dereva nikalichukua hadharani ili lolote likitokea nipate msaada.
“Nilikabidhiwa funguo za lile gari na documents zake, nikaondoka nalo hadi nyumbani kwangu. Kesho yake Dallas alimtuma mtu aniletee dola za Kimarekani 15,000 (zaidi ya Sh. milioni 24). Nilipouliza za nini aliniambia ni kwa ajili ya shopping ya kutembelea Harrier niachane na zile swaga za kwenye Noah (fedha inaongea). Kisha akanitumia cheni ya dhahabu.
“Siku iliyofuata alinitumia Sh. milioni 15 nipeleke nyumbani nikawaambie wazazi nimepata mchumba ambaye angeenda kujitambulisha baadaye. Niliwaambia ni Dallas ambaye walikiri kumfahamu kwa sababu alishawapigia simu na kujitambulisha kuwa ni mkwe wao.”
AMESHAKUTANA NA DALLAS?
“Hadi hapo nilikuwa sijamuona Dallas kwa sura na fedha nilikuwa natumiwa kila siku.
“Wakati hayo yakiendelea akaagiza nihamishiwe Mbezi Beach na kununuliwa lile gari lililoibua mzozo BMW X6.
“Nakumbuka siku niliyokabidhiwa lile gari nililia sana. Sikuamini macho yangu kwa sababu Dallas aliniambia amenitumia kazawadi kumbe ni BMW X6 (lina stori ndefu inakuja)!
“Kumbuka mwanzoni nilikuwa na boyfriend ambaye tulipendana sana lakini hatukupanga kufunga ndoa. Nilimweleza kila kitu akakubaliana na mimi japokuwa aliumia.
“Maskini! Kuanzia hapo nikawa nimeachana na yule boyfriend wangu lakini hakukuwa na namna kwa sababu niliamini nimepata mchumba wa kunioa.
ATAKIWA KUBADILI DINI
“Baadaye Dallas aliniambia nimeshakuwa mchumba wake hivyo nibadili dini. Kweli nilibadili nikawa Muislam na jina langu likawa Ilham. Hicho kilikuwa kipindi kigumu sana maishani mwangu kwa sababu nilionekana ni muasi katika dini yangu ambayo mama ni mzee wa usharika na mwimba kwaya, baba ni mtu wa kanisani sana.”
NINI KILIFUATA?
“Siku moja nilikuwa Tanga nashuti filamu, nilikuwa nikitoka hapo niende Morogoro. Dallas alinipigia simu akaniambia yupo Nairobi (Kenya) anakuja Tanzania. Nilimwambia nipo Tanga akaniambia atanifuata kule. “Niliendelea kupiga mzigo. Zilipita saa nyingi, baadaye nikiwa na kruu yangu, Dallas alinipigia simu akaniambia ameniona.
“Nilikataa, akaniambia namna nilivyo, nguo nilizovaa na watu niliokuwa nao, alipatia. Kumbe alikuja na Toyota Prado.
WOLPER MORO, DALLAS DAR
“Tulipomaliza kurekodi Tanga tulikwenda Morogoro, yeye aliniambia anaelekea Dar. Tulikuwa tunawasiliana. Nilipomaliza kurekodi Moro nilirejea Dar. Hapo ndipo vituko vikawa juu ya vituko.
“Niliambiwa mara kaonekana sehemu akiwa na mwanamke au wanawake. Mimi sikujali kwa sababu nilipomuuliza aliniambia hatuwezi kuonana kwa sababu kipindi hicho alikuwa katika swaumu hivyo akionana na mimi nitamharibia. (ulikuwa mwezi mtukufu).
BADO HAWAJAKUTANA?
“(Mguno) Hapo bado hatujakutana lakini yupo mjini na amejaa tele kwenye kumbi za starehe.
“Baada ya kumaliza swaumu, siku moja aliniambia anakuja nyumbani Mbezi Beach. Niliwaalika marafiki zangu tukapika vyakula, tukafanya usafi na kufukiza udi chumbani. Nilitandika mashuka meupe kitandani na kujipara kisha nikavaa ushungi kuanzia mchana nikakaa kama malkia nikimsubiri mchumba.
“Huwezi amini, hadi giza linaingia Dallas hakutia mguu. Nilipataje aibu kwa rafiki zangu waliotaka kumuona huyo mchumba? Ninyi acheni tu!
“Nilipomuuliza aliniambia alipata dharura kuna biashara alikuwa anafanya
HATIMAYE WAKUTANA LAKINI…
“Nilikasirika sana, nikasema huyu ni mchumba gani asiyetaka kuja kwangu? Nikampa muda wa siku tatu aje nyumbani na alete nguo zake zote. Kweli, siku ya tatu, asubuhi nilimsikia mtu akiita ‘Ilham Wolper Dallas’. Nilishajua sauti yake kupitia simu hivyo nilimkaribisha na nguo zake nikaingiza ndani. Lakini cha kushangaza alikuja na pikipiki!
“Alishinda nyumbani siku hiyo maana kuna ndugu zake walikuja. Hatukufanya chochote. Dallas aliishia kunibusu shavuni kisha jioni akaondoka.
“Mjini kukawa hakukaliki. Natumiwa picha akiwa na wanawake tofautitofauti. Mmoja wa wanawake hao niliambiwa eti ana ‘ngoma’! Jamani hii dunia ina kichaa!
“Muda ukasonga, vitimbi vikawa vingi. Dallas simuoni. Muda wa kukaa kwenye ile nyumba uliisha hivyo nikahama na nikamwambia akachukue nguo zake.
UCHUMBA WAVUNJIKA, SASA ANAPUMZIKA HAPA
“Baadaye uchumba ukavunjika tena mimi ndiyo nilimwambia simtaki tena. Nilikaa muda hadi baadaye nilipopata mwanaume wangu wa sasa. Anani-control vizuri kwa sababu kanipita umri na ana busara. Tunapendana sana. Najuta kumfahamu Dallas. Siwezi kusahau tukio hilo katika maisha yangu. Dallas alicheza na hisia za moyo wangu. (akaangua kilio) Niliteseka sana. Ni Mungu tu anajua…
VIPI KURUDIA UKRISTO?
“Nimekaa muda siendi kanisani. Nilikuwa najifungia ndani nalia kama mama yangu alivyokuwa anafanya. Siku moja nilimwambia mwanaume wangu akaniambia kuliko kulia kila siku bora nirudi kanisani. Ndipo nikarudia ukristo. Kwa sasa nasali Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Kijitonyama, Dar,” alisema.
MBALI NA DALLAS
Kwa mara ya kwanza Wolper alikubali kuorodhesha listi ya wanaume aliowahi kuwa nao kimapenzi kwa kuwachambua mmoja mmoja.
ALI KIBA
Bila kupepesa macho, Wolper alikiri kuwa msanii wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ndiye aliyemfundisha mapenzi: “Ni kitambo kidogo. Wote hatukuwa mastaa lakini yeye alifanikiwa kuchomoka. Kabla ya Ali (Kiba) nilikuwa na mwanaume lakini hatukuduu kwa maana ya utu uzima, ilikuwa yale ya kitoto. Lakini Ali ndiye hasa aliyeniingiza kwenye ulimwengu wa mapenzi.
KWA NINI WALIACHANA?
“Ali akawa staa. Alipokwenda nje nikasikia wanawake wanamshobokea. Sasa mimi sikutaka karaha nikakaa pembeni lakini jamaa ni mtu poa sana na tukikutana tunasalimiana freshi kabisa.”
DIAMOND VIPI?
“Ni kweli niliwahi kuwa na Diamond (msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul). Tulikuwa na uhusiano lakini pia alikuwa mshirika wa kibiashara (hataki kuitaja). Yeye alikuwa hawezi kulala bila kuniona, lakini tulikaa kama mwezi mmoja, kwa sasa amebaki kuwa rafiki yangu na siyo mpenzi tena kama zamani,” alisema Wolper.
VIPI KUHUSU JUX?
“Jux (msanii wa Bongo Fleva, Juma Khalid) nilikuwa naye kabla ya Dallas na yule mwanaume wangu niliyeachana naye wakati wa Dallas. Katika maisha yangu nilimpenda sana Jux. Siyo marioo ni mwanaume mtafutaji aliyejiamini. Kwa sasa sipo naye. Dallas pia alichangia mimi kuachana na Jux,” alimalizia Wolper ambaye kwa sasa ana mwanaume asiyependa kumwanika.

Jumatano, 27 Novemba 2013

ZITTO SASA AANZAKUWASHUGHULIKIA WALIO MCHAFUA

WAKATI Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kikimwandikia Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe barua ya kumtaka ajieleze dhidi ya tuhuma zinazomkabili, yeye ameamua kukimbilia polisi akimshitaki mmoja wa viongozi wenzake.


Habari za kuaminika zimedai kuwa Zitto ambaye hivi karibuni alivuliwa cheo chake cha unaibu katibu mkuu wa CHADEMA, inadaiwa amefungua mashitaka polisi akimtuhumu Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Dar es Salaam, Henry Kileo kwa madai ya kusambaza waraka katika mitandao ya kijamii.

Akithibitisha tukio hilo, wakili wa Kileo, Peter Kibatara, alisema kuwa mteja wake amemriwa kufika makao makuu ya Jeshi la Polisi leo Jumatano saa nane mchana na kuonana na mmoja wa maofisa wa juu wa jeshi hilo, aliyetajwa kwa jina moja tu la Mbutta, kufuatia mashitaka yaliyofunguliwa na Zitto dhidi yake.

Akizungumza kwa njia ya simu na mwandishi wetu, Kileo alikiri kuitwa polisi, ingawa alidai hajui ni waraka gani anaotuhumiwa kuusambaza unaomchafua Zitto.

“Kwa kweli sijui hata mimi ni waraka gani, ingawa hivi karibuni kulikuwa na waraka wa siri uliodaiwa kutoka CHADEMA, na ambao ulijaa tuhuma za usaliti. Lakini huo tuliishaukana siku nyingi. Labda kuna mwingine,” alisema Kileo.

Zitto kutwa nzima ya jana hakuweza kupatikana kwa njia ya simu kufafanua mashitaka aliyofungua polisi. Simu zake zote za kiganjani zilikuwa zimezimwa.

-Tanzania daima.

Super Nyota wa Mkoa Wa Dodoma atoa ya moyoni mwake

Haya ndio maneno ya kijana mwenye kipaji cha hali ya juu cha kutayarisha mziki na kuimba na ndo Super nyota wa mwaka 2013 Wa mkoa wa DODOMA JACKO BEAT aamua kuto ya moyoni soma mwenyewe
KWA YULE PRODUCER ANAEONGEA KUHUSU JACO BEATS NIMEPATA UJUMBE WAKO MIMI SINA SINA SHIDA NA WEWE KWANI SHIDA SI KUWA PRODUCER MKALI BALI NI KUTOA HEAT SONGS ZIVUKE BODA YA DODOMA KAMA KILAZA,MALAIKA NA I SAY AFU NDO UANZE KUNIPA CHALENGE ILA KWA MANENO YAKO UNAYOONGEA STUDIO HAYANIPI PRESHA NA YANAZIDI KUNIJENGA KWANI NAFRAHI SANA KUONA NAWAPA PRESHA TENA KILA SIKU KUBAKI MIDOMONI MWENU MIMI NAZIDI KUFANYA MAMBO JUU YA MAMBO NA BIG UP KWA MAPRODUCER WANAOFANYA HARAKATI KWENYE GEMU LA DOM KAMA
1.KID MAN
2.KIMAMBO
3.DABO
4.ABOUU
5.F THE BOY
6.BARNY
7.STEVE EE
8.LIL BELO
9.NOTY
10.PIN OUT
NA MA PRODUCER WOTE WANAOFANYA HARAKATI NA SIO KUONGEA MANENO YASIO NA FAIDA NA MZIKI WETU ILI MZIKI UFIKE MBALI
(DEDICATION SONG: YA MOYONI BY TOMPWINYO)

Jumatatu, 25 Novemba 2013

Pata link ya kuona Video ya Hotuba ya Zito Kabwe Kwa mara ya kwanza baada ya kuvuliwa uongozi

Zitto na Demokrasia

Zitto na Demokrasia

PRESS CONFERENCE VIDEOS: SITOKI CHADEMA-ZITTO

TAARIFA YA ZITTO ZUBERI KABWE (MB) KUHUSU KUVULIWA NAFASI ZA UONGOZI NDANI YA CHAMA CHANGU CHA CHADEMA
URL: http://www.youtube.com/zittokabwe

SITOKI CHADEMA


NITASIMAMA DAIMA MBELE YA DEMOKRASIA


NINAPOZUSHIWA NAUMIA MIMI NI BINADAMU


USAMBAZAJI WA RIPOTI YA SIRI KUHUSU ZITTO KABWE  


KUSHAWISHI WAGOMBEA WA CHADEMA KUJITOA KWENYE UCHAGUZI 2010
POSHO ZA WABUNGE


TAMKO LA PAC HESABU ZA VYAMA HAZIJAKAGULIWA CAG


TUHUMA ZINAZOMKABILI ZITTO ZUBERI KABWE KUTOMKAMPENIA RAIS WA CHADEMA KATIKA UCHAGUZI 2010


UJENZI WA CHADEMA KIGOMA


PRESS CONFERENCE – TUHUMA

Jumapili, 24 Novemba 2013

Kikwete atambua umuhimu wa Blogu katika kuisafisha nchi

Teteeni nchi badala ya kuiponda kwenye mablogu, Rais Kikwete Anena.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  • Teteeni nchi badala ya kuiponda kwenye mablogu, Rais Kikwete awaambia Watanzania 

Watanzania waishio nje Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema wajibu mkuu wa Watanzania wanaoishi nje ya nchi ni kuisemea vizuri, kuihangaikia na kuitetea nchi badala ya kushinda kwenye mablogu wakiiponda, kuibeza na kulalamika.

Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa kuishi kwa Watanzania nje ya nchi kutaonekana jambo la maana zaidi ikiwa watatumia rasilimali na fursa wanazozipata ugenini kusaidia kubadilisha hali na maisha ya ndugu zao waliobakia Tanzania.
Rais Kikwete pia amewaonya Watanzania hao wasije kuchanganyikiwa na kujichanganya wenyewe kwa kuiga tamaduni za kigeni kupita kiasi. 


 
Rais Kikwete alikuwa anazungumza na Watanzania waishio nchini Poland usiku wa juzi, Alhamisi, Novemba 21, 2013, kwenye Hoteli ya Bristol mjini Warsaw ambako alifikia wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku nne katika Poland.

Aliwaambia Watanzania hao na familia zao: “Matumaini na matarajio yetu sisi tuliobakia nyumbani ni kwamba mtaisemea
vizuri nchi yetu, mtaitetea nchi yenu, mtaihangaikia nchi na kuleta faida nyumbani. Ni jambo haliingii akilini kuwa baadhi
yenu mnaweza kuishi hapa na kazi yenu ikawa ni kushinda kwenye mablogu mkilaumu nchi yenu wenyewe. Nchi mbaya,
viongozi hawafai..mnapata faida gani. Mnazo nchi ngapi?”
Aliongeza Rais Kikwete: “Kuhangaikia nchi yetu ni wajibu wenu ambao hamwezi kuukwepa. Matumaini yetu ni kwamba
mtasukuma mbele maslahi ya nchi yenu, mtatetea ustawi wa nchi yenu na ndugu zenu. Fursa zilizoko hapa mnazijua
wenyewe, sisi hatuzijui. Nyie ndio mnaishi hapa, sisi tuko mbali na hatuwezi sisi kutegemewa na kutarajiwa tufanye
mambo ya hapa ambayo hatuyajui.”
Alisisitiza Rais Kikwete: “Mbona kazi za ma-Ngo’s mnazifanya vizuri bila kusukumwa ama kushawishiwa lakini
kazi za kusaidia ndugu zenu hamfanyi? Kama hata hamwezi kusaidia ndugu zenu mnachangia nini nchi yenu?”
Rais amesema kuwa kwa Watanzania waishio nje kuonekana wanajali na kutetea nchi yao kutasaidia kujenga hoja ya msingi kuhusu umuhimu wa kuanzishwa kwa uraia pacha (dual citizenship) ambao Watanzania waishio nje wanaulilia. “Mnaweza kuhalalisha hoja ya uraia pacha kwa kuwa watu wenye faida kwa nchi.”
Kuhusu ombi lao la uraia pacha, Rais Kikwete amesema kuwa ni wajibu wa Watanzania waishio nje kuongeza kasi ya kuchangia mjadala kuhusu suala hilo ili likubaliwe kuingizwa kwenye Katiba Mpya.
“Rasimu ya kwanza ya Katiba ililikataa jambo hilo kwa sababu hili ni jambo lisilokuwa na ushabiki na upenzi mwingi
nyumbani. Ujumbe wangu kwenu ni jipangeni vizuri kutetea hoja yenu hii. Saidieni mjadala wa jambo hilo badala ya
kushinda kwenye mablogu mkijadili siasa na hivyo kusahau yenye maslahi kwenu.”
Kuhusu kuiga tamaduni za nchi nyingine na kusahau za nyumbani, Rais Kikwete aliwaambia kuwa inaelekea kuwa baadhi
wachache wanaoishi nje ya nchi, wamejichanganya na kuchanganyikiwa kiasi cha kusahau mambo ya kwao.
Rais Kikwete alitoa kauli hiyo baada ya mmoja wa Watanzania kudai kuwa suala zima la mahari limepitwa na wakati na kuwa kutoa mahari ni sawa ni kuwauza watoto wa kike.
Rais ambaye alionyesha kushangazwa na kauli hiyo, alijibu: “Msiige mambo ya kigeni kiasi cha kuanza kuchanganyikiwa.”
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

Jumatatu, 11 Novemba 2013

ZITO ATOA TAMKO

TAMKO rasmi la Ndugu Zitto Z. KABWE (MB) kuhusiana na kinachoitwa "Taarifa ya Siri ya Chadema"





TAMKO rasmi la Ndugu Zitto Z. KABWE (MB) kuhusiana na kinachoitwa "Taarifa ya Siri ya Chadema"

Ndugu Wanahabari,

NILIPOKUWA katika ziara ya bara la Ulaya kati ya Oktoba 21 mpaka Novemba 2 mwaka huu (2013), nilipokea kwa njia ya barua pepe ripoti inayoitwa "Taarifa ya Siri ya Chadema" ambayo pia ilikuwa imesambazwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii.

“Taarifa ya Chadema inasema kwamba chama hicho (chama changu) kilikuwa kimechunguza mwenendo wangu tangu mwaka 2008 hadi 2010 na kubaini kuwa mimi napokea fedha kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kuivuruga Chadema.

Ripoti hiyo ilinihusisha pia na mwananchi raia wa Ujerumani, Andrea Cordes ambaye, kwa mujibu wa ripoti hiyo, alinisaidia kupokea na kuhifadhi kiasi cha dola 250,000 za Marekani kupitia kwenye akaunti yake binafsi.

Taarifa hii ya kutunga na iliyojaa uongo wa kiwango cha kutisha, imenifadhaisha, kunisikitisha na kunikasirisha.

Taarifa hii iliibuliwa katika kipindi ambacho nilikuwa safarini kutetea haki za Watanzania na Waafrika ambao utajiri wao wa rasilimali unafaidiwa na watu wachache waliohifadhi mali katika nje za nje na pia kupigania makampuni ya mataifa tajiri yalipe kodi stahiki katika nchi zetu.

Pengine lengo la ripoti hiyo lilikuwa ni kutaka kunipoteza kutoka katika nia na dhamira yangu ya dhati ya kutaka Watanzania wafaidike na utajiri wao. Muda ambao watunzi wa ripoti hiyo waliamua kutoa taarifa yao unazua maswali mengi kuliko majibu.

Nafahamu kwamba mimi ni mwanasiasa ambaye nimekuwa mlengwa (target) wa mashambulizi kutoka kwa makundi mbalimbali ya wanasiasa na vikundi vyao. Kama mwanasiasa, niko tayari kupokea changamoto zozote zinazokuja na uanasiasa wangu.

Hata hivyo, ambacho sitakubali ni kwa watu kutumia jina langu na uanasiasa wangu kunichafua mimi binafsi na watu wengine wasiohusika kwa sababu ya kutaka kutimiza malengo yao ya kidhalimu.

Raia huyo wa Kijerumani tayari amekana kuhifadhi fedha zangu. Kwa maelezo yake kwa baadhi ya viongozi wa Chadema amekana kuwa na akaunti inayotajwa na amekana pia kuwepo nchini Ujerumani katika siku na wakati uliotajwa kwenye ripoti hiyo.

Ripoti hiyo imemtaja pia mtu kama Dk. Charles Kimei, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB ikidai kwamba nilikutana naye na alishiriki kwenye igizo hilo la kunipa fedha.

Niseme mapema kwamba tangu kuzaliwa kwangu sijawahi hata mara moja kukutana na Dk. Kimei popote pale ndani au nje ya nchi. Kumuingiza mtu ambaye amejenga jina lake kwenye taaluma ya kibenki kwa sababu tu ya lengo ovu la kumchafua Zitto Zuberi Kabwe si uungwana bali ni unyama.

Kutokana na uchafuzi huu wa wazi dhidi ya taswira yangu binafsi na watu wengine walioingizwa kwenye mkumbo huu, nimeandika rasmi kwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk.Wilbrod Slaa kumwomba athibitishe kwamba kinachoitwa Taarifa ya Siri ya Chadema ni kweli ni taarifa ya chama au kiikanushe ili niweze kuchukua hatua za kisheria dhidi ya waandishi wa hekaya hiyo.

Cha ajabu, nimepokea ujumbe wa kutishiwa maisha kutoka kwa mtu anayejiita Theo Mutahaba na kuahidiwa KUPOTEZWA endapo nitaendelea na jitihada zangu za kupambana na ufisadi na kutafuta haki kwa Watanzania wote pasipo kujali tofauti zao za kiitikadi, kikanda, kikabila na kidini.

Natarajia kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya wote ambao wamehusika na utungaji na uenezi wa taarifa hii. Nitahakikisha kwamba wahusika wanatafutwa na kufunguliwa mashitaka stahiki ya upotoshaji na kuchafuana.

Ni matarajio yangu kwamba wale wenye mapenzi mema na Tanzania, mimi binafsi na utawala wa sheria, wataelewa nia yangu ya kutafuta haki katika suala hili.

Nimeamua kujitolea maisha yangu kwa ajili ya Watanzania na kama alivyopata kusema Rais Mstaafu wa Afrika Kusini, Nelson Mandela; “Struggle Is My Life.”

Forward Ever, Backward Never- Kwame Nkrumah

Zitto Kabwe (Mb)

10/11/2013

Theo Mutahaba amjibu Zitto Kwa Tamko alilolitoa leo


 
Theo Mutahaba amjibu Zitto
Ndg. Zitto
Nasikitishwa sana na hizi tabia zako za ajabu ajabu. Mimi nafanya kazi katika moja ya taasisi za ki usalama na nimeshirkia mara kadhaa kukupa fedha. Nyendo zako hata na sisi tunazijua na nimeshangazwa na utoto wako wa kuandika waraka ambao umetoa vitisho ambayo inadaiwa kutoka kwa Andrea Codes. Ndugu napenda kukuonya kwamba umefanya mengi ambayo hata wana Chadema hawajui.
· Swala la Bomu Arusha ulishiriki na lengo ilikuwa ni kumuua mwenyekiti wa Chadema pamoja na
Ndg. Lema. Hii kitu ulipanga, wewe, mwigulu na vyombo vya usalama ·Zitto, rais Kikwete alipoenda Sudan ya Kusini uliambatana naye. Unakumbuka sababu ya wewe kuitwa? Nikukumbushie kwamba ilikuwa zawadi kwako ya kuihujumu chadema. CCM hawakupendi, bali wanapenda hujuma zako ndio maana walikudanganya kwamba watakusaidia kupata uenyekiti CDM ikiwepo kumuua Mbowe na
kumdhoofisha Dr. Slaa
· Ndg. Zitto unadanganya umma kwamba unafuatilia fedha Uswisi wakati hii ni njama ambayo imesukwa na TISS kisha ukakabidhiwa ili CHADEMA isiibane sana serikali.
· Tueleze ni majina gani uliyoyapata. Na kama umeyapata, tunaomba kujua jina lako ni namba ngapi, kwa sababu na wewe una fedha nje ya nchi na ushahuidi tunao
· Umekuwa ukijenga mtandao wa kuwania uenyekiti na fedha ulizopewa na TISS pamoja na CCM ili kumn’goa Bw. Mbowe kwenye uenyekiti
wa CHADEMA ili 2015 CCM ishinde.
· Zitto, una ghorofa Dodoma karibu na St. Gasper Hotel. Fedha za kujenga lile jengo zimetoka wapi? · Zitto, Barrick gold walikujenga shule pale jimboni kwako. Baada ya lile shule kujengwa na pia kupewa kitita cha fedha ulinyamaza kabisa
· Ndg. Zitto, wakuu wengi wa mashirika ya umma wameleta malalamiko TISS kuhusu unavyochukua
fedha kwao. Hilo unalijua kama ni ufisadi?
Ndg. Zitto, wewe ni kijana mdogo. Hizi tamaa zako za kifisadi zitaipeleka nchi pabaya. Tunakuangalia na kelele zako hasa fedha za uswisi. Usichezee na akili za watanzania. Wewe ni fisadi namba moja.
Umeficha fedha nje, ama nikukumbushe kwamba, majuzi ulipokuwa nje ya nchi ulitoa fedha kwenye benki Fulani. Ile account umefunguliwa na nani?
Badilika kijana. Kisiasa umeshajimaliza. Pengine nikukumbushie kwamba mawasiliano yako na Jack Nzoka, Mwigulu, Ridhiwani za kisaliti ndio chanzo cha kuanguka kwako. Ila hacha kuwadanganya watanzania na kiini macho cha Uswisi. Umeshajua mengi sana , usishangae kijana ukija kutoweka ghafla. TISS hawachezi na mtu. Na ni wao au CCM ndio watakao kumaliza sio CHADEMA. Ule waraka unaosambaa ni mali ya TISS na imeratibiwa na CCM ambao ndio ndugu zako wakubwa Andrea, take care of your son. Get out of these Zitto corrupt acts. you know quite well that we wired you money and we have the evidence. Why would you waste your effort making noises? do you know the German government is investigating this matter? why would you fall for Zitto childish internet games of writing emails to the Chadema
leaders. So for your information, the document came from CCM and Tanzania Intelligence
Services Nakutakia kila la kheri kwenye kuhujumu Chadema.