Uteuzi huo unamrejesha Dk Migiro bungeni baada ya
kuondoka Januari 5, 2007 akiwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, alipoteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN)
na kuhudumu hadi alipomaliza muda wake Januari mwaka jana.
Baada ya kurejea nchini, Dk Migiro aliteuliwa kuwa
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Idara
ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa.
Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya
Rais jana, ilimnukuu Katibu Mkuu Kiongozi, Dk Florens Turuka akisema
uteuzi huo umeanza tangu juzi.
Uteuzi huo unatokana na mamlaka ya kikatiba aliyo
nayo Rais Kikwete ya kuteua wabunge 10.Mwanasiasa huyo aliyezaliwa Julai
9, 1956, aliwahi pia kuwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na
Watoto kuanzia mwaka 2000 hadi 2005.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni