SIMBA WATAKATA WACHUKUA MSHINDI JEMBE
7:10 PM
No comments
Wekundu
wa Msimbazi simba ya jijini Dar es Salaam leo imefanikiwa kwa mara
nyinge kuzima kidomo domo, mikogo na mbwe mbwe za kila namna za watani
wao wa jadi Yanga kwa kuwafunga magoli 3-1 katika mchezo maalum wa NANI
MTANI JEMBE mchezo uliopigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam hii
leo.
katika
mchezo huo Magoli ya simba yaliwekwa kimiani na mshambuliaji wake
mahiri mwenye kasi nyingi na mbinu lukuki za ufungaji Hamisi Tambwe
ambaye alipachika magoli 2 huku bao la tatu likifungwa na mchezaji
aliyesajiliwa dirisha dogo kutoka Mtibwa Awazi Juma huku goli la Yanga
likifungwa na Emmanuel Okwi.
Patashika ya kuwania mpira
Hali jukwaa la yanga ilikuwa si shwari sana...
Ngome hata iwaje ndio Simba walipita...
Simba wao ilikuwa shangwe tu.
CHANZO : FATHER KIDEVU
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni