Ijumaa, 31 Januari 2014

Morogoro kuamua kati ya Ofa ya usafiri na Maisha Bora kutoka kwa Wabunge wao

Selemani Msindi "Afande Sele // The king of Rymes" hapa akiwa jukwaani akiwapa neno wakazi wa MOROGORO katika mwendelezo wa mikutano ya CHADEMA chini ya Oparesheni Pamoja Daima (OPD),,, Wana Morogoro wao wameapa kumtema Aziz Abood ifikapo 2015,, Wameenda mbali zaid na kumsihi Abood Aziz aachie ngazi kabla ya 2015,, baadhi yao wamemshauri achukue kilicho chake na arudi kwao Uarabuni akalime Tende na Haluwa !! Km itashindikana basi aende Turiani kulima Miwa..... Habari za chini ya kapeti zinasema kuwa Ndugu Abood sasa Presha juu Aidha yeye aapa kuja na mbinu za kizembe ili kumpoteza Afande Sele,,, Asema atapunguza nauli kwenye mabasi yake Yafanyayo roote za MORO to DAR kutoka Tsh 7000 mpaka 2500 kwa wakazi wa MOROGORO tu,,,, Teh teh teh........

Alhamisi, 30 Januari 2014

TAMKO ALILOLITOA MZEE JOHN MALECELA JUU YA MWENENDO WA CCM

TAMKO ALILOLITOA MZEE JOHN MALECELA JUU YA MWENENDO WA CCM


Ndugu zangu waandishi wa habari, awali ya yote naomba niwasalimie na niwapongeze kwa kufika -mwaka mpya 2014, pia naomba niwapongeze kwa kazi kubwa ambayo mmekuwa mkiifanya hasa kuhakikisha watanzania wanapata habari kwa kila jambo linaloendelea kila kona ya taifa letu la Tanzania.

Ndugu waandishi wa habari nimewaita hapa ili kuzungumza nanyi na mnisaidie kufikisha ujumbe kwa watanzania hasa kuhusu jambo hili ambalo limekuwa gumzo kwa watanzania wengi la mbio za urais 2015 kwa baadhi ya watu ndani ya chama changu cha mapinduzi (CCM), kilichonisukuma zaidi na kupata hamu ya kuongea nanyi ni baada ya kumsikia -na kumuona kijana wetu ndani ya chama cha mapinduzi bwana Paul Makonda akiwa na ujasiri wa kukemea vitendo mambo haya yanayofanywa na baadhio ya viongozi bila uwoga wowote naomba tuchukue fursa hii kumpongeza sana kijana huyu.

Nadiriki kusema nampongeza kijana huyu hasa kwa kauli zake nzito na za kijasiri kwa maslahi ya chama changu cha CCM ili chama kiendelee kupendwa na kuchaguliwa na watanzania.

Pia itakuwa si busara kama sitawapongeza vijana wangu katibu mkuu wa chama ndugu ABDULRAHMAN KINANA na NAPE NNAUYE kwa juhudi zao za dhati za kujenga chama na kuendelea kuwaeleza wananchi juu ya misingi bora ya chama cha mapinduzi (CCM) kwa kuwakemea viongozi wasiofaa bila kujali cheo na umaarufu wao ndani ya chama na serikali, nawaomba waendelee -na juhudi zao hizo nami naziunga mkono juhudi zao na kama kuna watru wanaowabeza naomba wasijali kwani kukemea viongozi wasiofaa ndani ya chama na serikali ni msingi wa chama chochote kilichounda serikali.

Aidha nawaomba watanzania wenzangu wazalendo wasikubali kukatishwa tama na kikundi cha watu wachache wasio na mapenzi mema na taifa letu ambalo limekuwa mfano wa kuigwa kwa amani, upendo, utulivu na mshikamano urithi tulioachiwa na baba yetu wa taifa mwalimu julias kambarage nyerere ndani na nje ya mipaka ya bara letu la afrika.

Ndugu zangu waandishi wa habari naomba niwaambie kuwa msemaji wa UVCCM kijana wetu Paul Makonda namuunga mkono kwa -kitendo chake cha ujasiri cha kumkemea ndugu EDWARD NGOYAI LOWASSA bila uwoga kwa jinsi anavyokivuruga chama chetu kwa lengo la kutaka urais 2015 huku secretariet ya chama ikiwa imekaa kimya wakati inajua kuwa muda wa kuanza mbio hizi bado na kufanya hivi kwa sasa ni kukiuka misingi na katiba -ya chama. Hapa najiuliza kuwa ile misingi imara ya uongozi ndani ya chama chetu cha mapinduzi iko wapi? Mpaka tumuachie mototo ndio akemee haya? Je, hapa chama kiko wapi?

Ukweli ni kwamba wanachama wetu na vijana wamekuwa njia panda huku wakitamani kusikia tamko au karipio la chama juu ya suala hili la harakati za urais 2015 bila mafanikio.

Naomba niseme kuwa bila kuwa na karipio au tamko la chama, hawa wanaotumia pesa zao hadharani kwa lengo la kutafuta umaarufu na ushawishi kwa vijana ili kupata madaraka wanaharibu misingi yetu bora ya uongozi iliyowekwa na waasisi wetu ndani ya chama.

Kinachonisikitisha zaidi ni kuona juhudu za uongozi wa sasa wa chama ngazi ya juu ikiwa ni pamoja na sekretarieti inayoongozwa na katibu mkuu ABDULRAHMANI KINANA na katibu mwenezi NAPE NNAUYE za kutetea chama hiki zinatiwa mchanga.

Ninaomba juhudi hizi zisibezwe na watu wenye nia njema na chama. Ukweli ni kwamba vijana hawa wamekuwa na juhudi kubwa sana ya kujenga na kuimarisha chama chetu -kwa wananchi kila pembe ya taifa letu kwa kukemea na kueleza misingi ya uongozi bora. Swali: Je! Chama hakioni haya mpaka vijana ndio waone?

Kwa hili ni lazima tubadilike ili kujenga chama chetu na naishauri -secretariet ya chama lazima ichukue hatua mara moja, kijana huyu paul makonda asingesema haya yote kama hana uhakika wa ushahidi wa wa haya aliyoyasema na nampongeza sana.

Vijana na wanachama wengi wa CCM wamekuwa na hamu kwa muda mrefu ya kutaka kujua msimamo wa chama chao bila mafanikio na ndio sababu ya baadhi ya-wengine kupoteza mwelekeo.

Sisi tulikijenga chama hiki kwa taabu sana hapakuwa hata mtu mmoja aliyediriki kutumia fedha zake kutaka madaraka. 

Nidhamu, busara na uchungu wa rasilimali za taifa hili kwa maslahi ya wananchi ndio vilituongoza kufuata misingi na maadili ya uongozi ndani ya chama na serikali, ndio maana tunaumia sana kuona chama sasa kinataka kutekwa na wenye fedha kwa uchu wa madaraka, mpaka tunashangaa na kujiuliza hizi pesa wanatoa wapi? Na haya madaraka wanayotaka kwa kununua ni kwa maslahi ya nani? Huku watanzania wakiendelea kuwa maskini.

Mfano hivi karibuni baadhi ya viongozi wa chama ngazi ya juu wamejibishana kwenye vyombo vya habari,vitendo hivi havina tija kwa chama na wala havileti umoja na mshikamano ambao umedumu ndani chama kwa muda mrefu.

Mwisho Ninaomba sekretarieti ichukue hatua haraka kama alivyoomba kijana wetu makonda na kweli kuchelewa kuchukua hatua jambo hili kumejionyesha wazi kwamba utaleta kutokuelewana ndani ya chama kusiko kuwa na lazima.

JOHN SAMWELI MALECELA
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
You might also like:

Jumapili, 26 Januari 2014

Tazama Mtazamo wa watu wa Mbeya juu ya Zitto kabwe CHADEMA

Chanzo cha habari   nikutoka kwa  mtu aliehudhuria kwenye mkutano na kupost facebook
 
MOJA YA TUKIO LILILOMUOGOPESHA DR SLAA...;

KWELI MBEYA HATUSHABIKII MTU, TUNASHABIKIA TAASISI YETU KWA MIOYO YETU ILIYOJAA UZALENDO.

HEBU LITAZAME JENEZA LA MSALITI ZITTO KABWE, AMBALO WANA MBEYA WAMEAMUA KUMFIKISHIA UJUMBE MZITO KWAMBA HAWAKUBALIANI NA UPUMBAVU NA UJINGA ALIOUFANYA.

  • 14 people like this.
  • Hance Patrick Mbey Huw Hawampendi Mtu Msalti Ndio Maana Wameamua Kufanya Ivo Kwamba Hawamhtja Huyo Msaliti
  • Abedinergo Peter KWANZA ZITO KABWE NI MCHAWI HAKUNA ASIYEJUA HILO. AMEWALOGA VIJANA WAPUMBAVU WA CCM KAMA AKINA #NTAHO NA #KAREEM ETI WAMSHABIKIE. PUMBAVU ZENU KAMA MNAMTAKA ZZK C MUMUWEKE CCM??? MNANG'ANG'ANA KTK NDOA ISIYOWAHUSU MBWA NYIE. INGIE BASI NA NYIE MZALISHWE, EEE C NDO MNATAKA. HATUMTAKI ZITO COZ NI ZIGO ZAIDI YA ZIGO LA MAVI.
  • Nelly Felix Usaliti ni mbaya sana ulimuua Yuda kabla hata ya aliesalitiwa kufa, Sikuzote msaliti wa siasa ufa kisiasa kama jamaa alivyojimalza mwenyewe kwa kupenda vya kuongwa.

Ijumaa, 24 Januari 2014

Magufuli Nomaa hajiwekea historia Dumila Haijawahi kutokea hii

TAZAMA PICHA..!!HIVI NDIVYO WAZIRI MAGUFULI ALIVYOSIMAMIA UJENZI W DARAJA LA DUMILA LILILOSOMBWA NA MAJI HUKO MOROGORO..JIONEE MWENYEWE HAPA



Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli akiwa katika gari linaloendelea na ujenzi wa daraja la Dumila.


Waziri Magufuli akitoa maelekezo kwa watendaji wa Tanroads.
Sehemu ya barabara iliyozolewa na maji ya mto Mkundi.
Waziri wa Ujenzi akikagua maeneo yaliyoharibika.
Dk. Magufuli akiendelea na kazi katika daraja hilo.
Kazi za ujenzi zikiendelea eneo hilo la daraja lililoharibika.
Dk. Magufuli akiwapa hi mafundi wanaoendelea na ujenzi wa daraja hilo.

WAZIRI wa Ujenzi, Dk. John Pombe Magufuli amepiga kambi mkoani Morogoro kusimamia mwenyewe ujenzi wa Daraja la Dumila ambalo ni kiungo muhimu cha barabara ya Dodoma – Morogoro lililosombwa na mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia tarehe 22.01.2014 na kusababisha magari kutopita kabisa ama yanayotoka upande wa Dodoma au Morogoro. Mbaya zaidi hakuna njia nyingine mbadala zaidi ya hiyo.
 Posted By: A mzalendo source mzalendo bogspot.com

Alhamisi, 16 Januari 2014

Pinda atatua Mapigano ya wakulima na Wafugaji mkoani Manyara









Waziri mkuu wa Jamuhuri ya Muungano waTanzania mheshimiwa Mizengo Pinda Leo katika wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara amezungumza na wakulima pamoja na wafugaji waliokuwa wakipigana kwaajili ya maeneno ambayo Serikali inadai kuwa ni hifadhi ya wanyama na mali asili
 Wafugaji wenye asili ya kimasai wao wanawafukuza wakulima kwamadai kuwa wakulima wanaharibu mazingira na ndomana serikali inawataka wote watoke katika hifadhi hiyo,  pia na wao wao wanakosa maeneo ya malisho kwaajili ya mifugo yao.
 Leo akiongea na Wakulima pamoja na Wafugaji hao Waziri mkuu ametaka hekima na utaratibu mzuri ufuatwe katika kuwahamishwaji wa wakulima na wafugaji. Pia akaeleza kuwa kama eneo hilo ni hifadhi na vijiji vyote vinavyo zunguka eneo hilo viliridhia basi si mfugaji wala mkulima mwenye haki ya kufanya shughuli  yoyote ile katika eneo hilo. Lakini kama vijiji havikuridhia katika uhamishaji wa eneo hilo na kulifanya kuwa hifadhi Basi wakae wajadili kwa pamoja na eneo hilo lirudishwe mikononi mwa wana vijiji hao.
Hadi mwisho wa mkutano huo hakuruhusu wakulima   kuendelea kulima wala wafugaji kuendelea kufuga katika maeneo hayo na kuona kama wao ndo wanao stahili kuwepo hapo. Nakutaka mapigano yasiwepo tena
Mungu ibariki Tanzania Mungu ibariki Afrika.

Korumba Mtanzania: Vijimambo special

Korumba Mtanzania: Vijimambo special:                       Hii ndio katuni kali zaidi ya wiki hii

Hisia za wakulima Wanaolima Kiteto mkoani Manyara







                                              Mkulima Francesco Lwiwa  ana haya ya kusema
"Ndugu zangu watanzania kuna jambo linanitatiza sana,ss hivi ni kipindi cha kilimo hasa kwa wale waloamua kujiajiri kupitia kilimo.Watu mbalimbali baada ya serikali kujenga soko la mahindi la kimataifa Kibaigwa walishawishika kutafuta maeneo mazuri yafaayo kwa kilimo.Watu wakaenda kwa wamiliki wa maeneo huko Kiteto wakanunua japo wengine tunakodi kwa hao masai wa kiteteto.From no where sirikali ya kiteto ikaja kuwapiga stop kulima kwa madai kuna hifadhi. Huku nakule watu wakaanza kuvunjiwa nyumba zao. Nakutakiwa watu waondoke lakini masai wakachangishwa fedha ya kusaidia kuondoa wakulima.Tatizo linaanzia hapa kutokana namisuguano nawakulima kulifikisha kwa waziri mkuu ilibidi afike ktk maeneo husika na kusitisha kuondolewa wakulima kwa madai hiyi hifadhi haitambuliki hivyo c sahihi kuwaondoa wakulima.Chaajabu mkuu wa mkoa,mkuu wa wilaya,mbunge na mkurugenzi wakapinga kauli ya waziri mkuu na kupelea sasahivi ni masai kuwafanyia mauaji wakulima kamamlivyoona kwenye vyombo vya habari ni ukweli mtupu jamaa Wamepewa claha za ajabu na jana kuna wakulima c chini ya ishirini wameuawa na matukio kama haya yamekua yakijiri kwa zaidi ya mwezi na wtu wamekimbia masha na tuliofanikiwa kulima hatujui hatima ya mashamba yetu .wtz ni ninihatima ya maisha yetu na uchumi wetu?kwani serikali gesi wamepewa wageni ardhi wageni ndo kipaumbele chao miradi mingi ni wazungu na wachina ,hii inayo jiita serikali ckivu ni kwa watu gani na hawa jamaa wanaongoza nani kama wapigakura wao wanakufa hatujackia tmko la kiongozi yoyote inatia huzuni BBC wanajua lakin hao mawazi hadi mkuu anajua hii jaman it's too much imetosha tusubiriane 2015 kitaakacho jiri"
  Wengine pia ambao hawakuwa tayari kutaja majina yao wanailaumu serikali hasa uongozi mzima wa mkoa wa manyara chini ya mkuu wa mkoa wake kwa kuonekana wanawajali sana wafugaji wa asili ya kimasai ambao wao wanaonekana kama ndo wenye haki ya kuyamiliki maeneo yanayo gombaniwa ambayo yanadaiwa ni ya hifadhi ya Mulitongos.

Bakamaza arudi tena kivingine 2014

Korumba Mtanzania: Michezo na Burudani: Bakamaza arudi tena kivingine 2014 Erick Backamaza Yule muandaaji Bora wa Video na Filamu mkoani Dodoma kwa ...

Jumatano, 15 Januari 2014

TABIA 10 ZITAKAZOKUFANYA UENDELEE KUBAKI KUWA MASKINI

TABIA 10 ZITAKAZOKUFANYA UENDELEE KUBAKI KUWA MASKINI

Umaskini ni hali ya ukosefu wa mahitaji ya binadamu ya msingi kama vile chakula, maji masafi, huduma za afya, mavazi na nyumba kutokana na kukosa uwezo wa kuvinunua. Hii pia inajulikana kama umaskini uliokithiri au ufukara. Umaskini wa kadri ni wa kuwa na raslimali chache zaidi au mapato madogo zaidi ikilinganishwa na watu wengine katika jamii au nchi au ikilinganishwa na hali ya kadiri duniani. Hali hii pia hujulikana kama umaskini halisi au unyonge. Umaskini linganishi ni hali ya kuwa na rasilimali chache au kipato cha chini kuliko wengine kwenye jamii au nchini, au ikilinganishwa na wastani duniani kote.

VIASHIRIA VYA UMASIKINI
Viashiria vya umasikini nchini tanzania ni kama kutokujua kusoma na kuandika, uhaba wa maji safi na salama, huduma duni za afya, vifo vingi vya watu, muda mfupi wa maisha, utapiamlo kwa watoto na watu wazima, ukosefu wa ajira, hali duni za maisha, kutofahamu vitu muhimu vya jamii.

MADHARA YA UMASIKINI
umasikini una madhara makubwa sana katika jamii mfano mmomonyoko wa maadili, ukosefu wa amani na utulivu, afya duni na vifo,

TABIA ZIPELEKEAZO UMASIKINI.
1. Usipende kuamka mapema, endelea kujigeuza geuza na kupiga miayo kitandani, kwani kama hakuna papasi au viroboto, una haraka gani kuwahi kuamka?

2. Usipangilie namna ya kutumia fedha zako. Upatapo fedha tu, we zitumie hapo hapo na zikiisha wala usifikirie jinsi ulivyozitumia. Kesho itajijua yenyewe.

3. Usiwaze mambo ya kuhifahi fedha benki, subiri hadi uwe na mamilioni, kwanza uta ‘save’ vipi wakati unamahitaji mengi? Hao wanaokushauri uweke fedha benki hawakuonei huruma na mahitaji yako.

4. Kamwe usijishuhulishe katika zile shughuli nyingine ambazo unaziita za wasioenda shule. Yani we msomi wa chuo kikuu unafanya biashara ndogo ndongo au kuwa na mifugo au shamba? Hizo ni kwa wale wasiojua shule.

5. Usifikirie kuanzisha biashara hadi malaika atoke mbinguni akuletee mtaji. Kwanza utaweza vipi wakati huna mamilioni? Kwanza wewe hauko ‘level’ moja na hao wanaoanzisha vibiashara vya hela ndogo. We ni wa muhimu sana.

6. Laumu kila kitu, laumu serikali, laumu mabenki, kwa kutokukopesha fedha, laumu saccos pia kwa kuwa fedha zinazowekwa huko zaweza kuibiwa au kuliwa. Laumu bosi au mwajiri wako kwa kutokupa mshahara mkubwa wa kuweza kuwekeza.

7. Tumia zaidi ya mapato yako ili kulifanikisha jambo hili, nunua zaidi vitu vya matumizi kwa mkopo, na azima fedha kwa marafiki na ikiwezekana mkope hata mwajiri (si utakatwa kidogo kidogo kwenye mshahara?), kama mwajiri hataki kukukopa, basi mwombe mshahara wa awali (advance salary) ili uweze kujinunulia unachotaka kama vile simu ya bei ghali, macheni, mapete, mahereni ya dhahabu n.k. Maisha yenyewe mafupi inabidi ujifurahishe.

8. Fanya ushindani na mavazi ya bei kubwa, hakikisha unavaa nguo zilizo katika chati kuliko wafanyakazi wenzako au rafiki zako wote. Wakati wowote jirani au rafiki yako anaponunua simu wewe nenda kanunue ya gharama zaidi yake ili umkomeshe akuheshimu.

9. Jinunulie gari zuri na la kifahari ambalo linagharimu mara tatu ya mshahara wako wa mwaka mzima. Hii itakusaidia kukuweka muda mrefu ukilipa deni la gari na sio shughuli nyingine za maendeleo.

10. wape watoto wako kila kitu wanachohitaji, kwa sababu wewe ni mzazi mzuri unayejali, usiwaache wahangaike kupata chochote wakati wewe upo hai kwa ajili yao mtoto hakui kwa mzazi bwana! Kwa hali hii watafanikiwa kukua wakiwa wazembe, wavivu na hivyo kuwa masikini kiasi ambacho hawataweza kukujali katika uzee wako.

UKIFUATA HIZI KANUNI LAZIMA UTAFANIKIWA KUUKARIBISHA UMASKINI ULIO THABITI NYUMBANI KWAKO

Jumatatu, 13 Januari 2014

Korumba Mtanzania: Manyara Vita ya wakulima na Wamasai vyachukua sura...

 Manyara Vita ya wakulima na Wamasai vyachukua sura...: TUNAOMBA RAHI KWA PICHA::MAUAJI YA KUTISHA YATOKEA TENA KITETO MKOANI MANYARA MZAHA na uzembe un...

Manyara Vita ya wakulima na Wamasai vyachukua sura Mpya

TUNAOMBA RAHI KWA PICHA::MAUAJI YA KUTISHA YATOKEA TENA KITETO MKOANI MANYARA












MZAHA na uzembe unaodaiwa kufanywa na baadhi ya viongozi wilayani Kiteto na mkoani Manyara katika kusuluhisha mgogoro wa wafugaji na wakulima, umesababisha mauaji ya watu zaidi ya 13 usiku wa kuamkia jana.

Mbali ya vifo hivyo, vita hiyo iliyaonza majira ya saa 11 alfajiri kwa kutumia silaha za moto na jadi, imesababisha majeruhi zaidi ya 50 huku wengine wakiachwa na ulemavu wa kudumu.
Baadhi ya wakulima waliozungumza na gazeti hili jana, walisema wafugaji wa jamii ya Kimasai walivamia nyumba zao alfajiri ya kuamkia jana na kuzichoma moto, huku wakitoa kipigo kwa kila mtu waliyemuona mbele yao.
Habari hizo zinasema wakulima waliokuwa wabishi na kujaribu kupambana na kundi hilo la wafugaji wa Kimasai, walipigwa risasi na kupoteza maisha.
Hali ya baadhi ya vijiji wilaya Kiteto ilionekana kama uwanja wa vita kwani milio ya risasi na milipuko ya moto ilisikika kila kona.
Kuona hivyo, baadhi ya familia hasa wanawake na watoto, walilazimika kukimbilia porini ambako wafugaji hao waliwafuata na kuwaua.
Taarifa za awali zilizotolewa na wakulima zilisema kuwa mapigano hayo sasa yameingia katika hatua mbaya kwani kuna kundi kubwa la jamii ya wafugaji wa Kimasai wakiwa na silaha za kivita.
Mmoja wa wakulima, Machite, alisema eneo la Laitimi lenye wakulima wengi, ndilo lililoathirika zaidi na mapigano hayo.

“Sasa ngogoro huu unazidi kukua na unazidi kutumaliza sana na hiyo inasabaishwa na viongozi kupokea rushwa kutoka kwa wafugaji kwa madai kuwa watawafukuza wakulima ili Wamasai wachunge mifugo yao.
“Juzi tulifanya mkutano na Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Erasto Mbwilo juu ya kutatua migogoro na mfugaji mmoja wa Kimasai alieleza kuwa kiongozi mmoja wilayani Kiteto anachangisha fedha kwa ajili ya kuwapa maeneo ya kuchungia,” alisema.
Akizungumzia mgogoro huo, Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai, alisema tangu kuanza kwa mapigano hadi sasa watu zaidi ya 20 wamepoteza maisha.
Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Mkilamali Mpwapwa, alisema idadi ya waliofariki ambao miili yao imeshapatikana ni sita, lakini kuna uwezekano wa kuwapo wengine porini, hivyo wanaendelea kuwatafuta.
Kamanda huyo alisema bado wanafanya tathimini kujua idadi ya nyumba zilizochomwa na hasara iliyopatikana.
Alisema jeshi lake limeimarisha ulinzi na linawasaka wanaodaiwa kuhusika na mauaji hayo.