Alhamisi, 16 Januari 2014

Hisia za wakulima Wanaolima Kiteto mkoani Manyara







                                              Mkulima Francesco Lwiwa  ana haya ya kusema
"Ndugu zangu watanzania kuna jambo linanitatiza sana,ss hivi ni kipindi cha kilimo hasa kwa wale waloamua kujiajiri kupitia kilimo.Watu mbalimbali baada ya serikali kujenga soko la mahindi la kimataifa Kibaigwa walishawishika kutafuta maeneo mazuri yafaayo kwa kilimo.Watu wakaenda kwa wamiliki wa maeneo huko Kiteto wakanunua japo wengine tunakodi kwa hao masai wa kiteteto.From no where sirikali ya kiteto ikaja kuwapiga stop kulima kwa madai kuna hifadhi. Huku nakule watu wakaanza kuvunjiwa nyumba zao. Nakutakiwa watu waondoke lakini masai wakachangishwa fedha ya kusaidia kuondoa wakulima.Tatizo linaanzia hapa kutokana namisuguano nawakulima kulifikisha kwa waziri mkuu ilibidi afike ktk maeneo husika na kusitisha kuondolewa wakulima kwa madai hiyi hifadhi haitambuliki hivyo c sahihi kuwaondoa wakulima.Chaajabu mkuu wa mkoa,mkuu wa wilaya,mbunge na mkurugenzi wakapinga kauli ya waziri mkuu na kupelea sasahivi ni masai kuwafanyia mauaji wakulima kamamlivyoona kwenye vyombo vya habari ni ukweli mtupu jamaa Wamepewa claha za ajabu na jana kuna wakulima c chini ya ishirini wameuawa na matukio kama haya yamekua yakijiri kwa zaidi ya mwezi na wtu wamekimbia masha na tuliofanikiwa kulima hatujui hatima ya mashamba yetu .wtz ni ninihatima ya maisha yetu na uchumi wetu?kwani serikali gesi wamepewa wageni ardhi wageni ndo kipaumbele chao miradi mingi ni wazungu na wachina ,hii inayo jiita serikali ckivu ni kwa watu gani na hawa jamaa wanaongoza nani kama wapigakura wao wanakufa hatujackia tmko la kiongozi yoyote inatia huzuni BBC wanajua lakin hao mawazi hadi mkuu anajua hii jaman it's too much imetosha tusubiriane 2015 kitaakacho jiri"
  Wengine pia ambao hawakuwa tayari kutaja majina yao wanailaumu serikali hasa uongozi mzima wa mkoa wa manyara chini ya mkuu wa mkoa wake kwa kuonekana wanawajali sana wafugaji wa asili ya kimasai ambao wao wanaonekana kama ndo wenye haki ya kuyamiliki maeneo yanayo gombaniwa ambayo yanadaiwa ni ya hifadhi ya Mulitongos.

Hakuna maoni: