Waziri mkuu wa Jamuhuri ya Muungano waTanzania mheshimiwa
Mizengo Pinda Leo katika wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara amezungumza na
wakulima pamoja na wafugaji waliokuwa wakipigana kwaajili ya maeneno ambayo
Serikali inadai kuwa ni hifadhi ya wanyama na mali asili
Wafugaji wenye asili
ya kimasai wao wanawafukuza wakulima kwamadai kuwa wakulima wanaharibu
mazingira na ndomana serikali inawataka wote watoke katika hifadhi hiyo, pia na wao wao wanakosa maeneo ya malisho
kwaajili ya mifugo yao.
Leo akiongea na Wakulima
pamoja na Wafugaji hao Waziri mkuu ametaka hekima na utaratibu mzuri ufuatwe
katika kuwahamishwaji wa wakulima na wafugaji. Pia akaeleza kuwa kama eneo hilo
ni hifadhi na vijiji vyote vinavyo zunguka eneo hilo viliridhia basi si mfugaji
wala mkulima mwenye haki ya kufanya shughuli yoyote ile katika eneo hilo. Lakini kama
vijiji havikuridhia katika uhamishaji wa eneo hilo na kulifanya kuwa hifadhi
Basi wakae wajadili kwa pamoja na eneo hilo lirudishwe mikononi mwa wana vijiji
hao.
Hadi mwisho wa mkutano huo hakuruhusu wakulima kuendelea kulima wala wafugaji kuendelea
kufuga katika maeneo hayo na kuona kama wao ndo wanao stahili kuwepo hapo. Nakutaka mapigano yasiwepo tena
Mungu ibariki Tanzania Mungu ibariki Afrika.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni