Jumatano, 15 Januari 2014

TABIA 10 ZITAKAZOKUFANYA UENDELEE KUBAKI KUWA MASKINI

TABIA 10 ZITAKAZOKUFANYA UENDELEE KUBAKI KUWA MASKINI

Umaskini ni hali ya ukosefu wa mahitaji ya binadamu ya msingi kama vile chakula, maji masafi, huduma za afya, mavazi na nyumba kutokana na kukosa uwezo wa kuvinunua. Hii pia inajulikana kama umaskini uliokithiri au ufukara. Umaskini wa kadri ni wa kuwa na raslimali chache zaidi au mapato madogo zaidi ikilinganishwa na watu wengine katika jamii au nchi au ikilinganishwa na hali ya kadiri duniani. Hali hii pia hujulikana kama umaskini halisi au unyonge. Umaskini linganishi ni hali ya kuwa na rasilimali chache au kipato cha chini kuliko wengine kwenye jamii au nchini, au ikilinganishwa na wastani duniani kote.

VIASHIRIA VYA UMASIKINI
Viashiria vya umasikini nchini tanzania ni kama kutokujua kusoma na kuandika, uhaba wa maji safi na salama, huduma duni za afya, vifo vingi vya watu, muda mfupi wa maisha, utapiamlo kwa watoto na watu wazima, ukosefu wa ajira, hali duni za maisha, kutofahamu vitu muhimu vya jamii.

MADHARA YA UMASIKINI
umasikini una madhara makubwa sana katika jamii mfano mmomonyoko wa maadili, ukosefu wa amani na utulivu, afya duni na vifo,

TABIA ZIPELEKEAZO UMASIKINI.
1. Usipende kuamka mapema, endelea kujigeuza geuza na kupiga miayo kitandani, kwani kama hakuna papasi au viroboto, una haraka gani kuwahi kuamka?

2. Usipangilie namna ya kutumia fedha zako. Upatapo fedha tu, we zitumie hapo hapo na zikiisha wala usifikirie jinsi ulivyozitumia. Kesho itajijua yenyewe.

3. Usiwaze mambo ya kuhifahi fedha benki, subiri hadi uwe na mamilioni, kwanza uta ‘save’ vipi wakati unamahitaji mengi? Hao wanaokushauri uweke fedha benki hawakuonei huruma na mahitaji yako.

4. Kamwe usijishuhulishe katika zile shughuli nyingine ambazo unaziita za wasioenda shule. Yani we msomi wa chuo kikuu unafanya biashara ndogo ndongo au kuwa na mifugo au shamba? Hizo ni kwa wale wasiojua shule.

5. Usifikirie kuanzisha biashara hadi malaika atoke mbinguni akuletee mtaji. Kwanza utaweza vipi wakati huna mamilioni? Kwanza wewe hauko ‘level’ moja na hao wanaoanzisha vibiashara vya hela ndogo. We ni wa muhimu sana.

6. Laumu kila kitu, laumu serikali, laumu mabenki, kwa kutokukopesha fedha, laumu saccos pia kwa kuwa fedha zinazowekwa huko zaweza kuibiwa au kuliwa. Laumu bosi au mwajiri wako kwa kutokupa mshahara mkubwa wa kuweza kuwekeza.

7. Tumia zaidi ya mapato yako ili kulifanikisha jambo hili, nunua zaidi vitu vya matumizi kwa mkopo, na azima fedha kwa marafiki na ikiwezekana mkope hata mwajiri (si utakatwa kidogo kidogo kwenye mshahara?), kama mwajiri hataki kukukopa, basi mwombe mshahara wa awali (advance salary) ili uweze kujinunulia unachotaka kama vile simu ya bei ghali, macheni, mapete, mahereni ya dhahabu n.k. Maisha yenyewe mafupi inabidi ujifurahishe.

8. Fanya ushindani na mavazi ya bei kubwa, hakikisha unavaa nguo zilizo katika chati kuliko wafanyakazi wenzako au rafiki zako wote. Wakati wowote jirani au rafiki yako anaponunua simu wewe nenda kanunue ya gharama zaidi yake ili umkomeshe akuheshimu.

9. Jinunulie gari zuri na la kifahari ambalo linagharimu mara tatu ya mshahara wako wa mwaka mzima. Hii itakusaidia kukuweka muda mrefu ukilipa deni la gari na sio shughuli nyingine za maendeleo.

10. wape watoto wako kila kitu wanachohitaji, kwa sababu wewe ni mzazi mzuri unayejali, usiwaache wahangaike kupata chochote wakati wewe upo hai kwa ajili yao mtoto hakui kwa mzazi bwana! Kwa hali hii watafanikiwa kukua wakiwa wazembe, wavivu na hivyo kuwa masikini kiasi ambacho hawataweza kukujali katika uzee wako.

UKIFUATA HIZI KANUNI LAZIMA UTAFANIKIWA KUUKARIBISHA UMASKINI ULIO THABITI NYUMBANI KWAKO

Hakuna maoni: