Madudu (5) matano ya Wizara ya Elimu yaliyo weka historia Duniani mwaka 2013/2014
Mwaka 2013 na
2014 umekuwa ni mwaka wenye maajabu ya
madudu ambayo hayajawahi kutokea katika sekta ya elimu Tanzania.Maajabu hayo nikama
yafuatayo
1.MATOKEO
Kutangaza matokeo ya kidato channe ya mwaka 2013/2014 kwa
viwango vipya vya madaraja ya ufaulu yaliyo pingwa sana na watanzania na
Wabunge bungeni Kabla yakutumika kwa
kuwa viwango hivyo ambavyo havileti
maendeleo katika sekta ya elimu zaidi ya kudhorotesha sekta ya elimu Tanzania.
2.Ajira
27/2/2014 Wizara kupitia gazeti la Tanzania Daima ilitangaza
kuwa imewaajiri walimu 360000 bila kutoa majina ya walimu hao na ambao
wameajiriwa kitu ambacho hakikuwahi kutokea tangu Wizara hiyo ilipoanzishwa.
3.Mazoezi ya Vitendo
Mazoezi ya vitendo kwa walimu Tarajari waliopo vyuoni
haijawahi kutokea wakachelewa kwenda kwenye mazoezi hayo ya vitendo kama ilivo
sasa mwezi wapili unaisha bado tu wapo vyuoni bila sababu za maana.
4.Kusoma nakuandika
Haijawahi kusikika
Duniani kote kuwa kuna wanafunzi wanaomaliza shule ya msingi na kufanya
mitihani kisha kufaulukuendelea na
wanapoenda shule ya upili yaani secondari washindwe kusoma na kuandika lakini
kwa Tanzania hilo lime tokea na limesha zoeleka na kuwa kama kitu cha kawaida
tu.
5.Tovuti
Mwisho kabisa ukiingia kwenye tovuti yao ya wizara ya Elimu
kunasehemu ya kutoa maoni ya Yule anaetazama tovuti hiyo watu wengi wamekuwa
wakitoa maoni kuwa mfumo ni mbovu kwa zaidi ya 48% Kitu ambacho ni ajabu kutokea kwa nchi
nyingine pia tovuti hiyo haivutii kila siku vitu nivilevile.
INCHI YENYE UTAWALA BORA HAIWEZI KUWA NA ELIMU MBOVU