Ijumaa, 28 Februari 2014

Madudu (5) matano ya Wizara ya Elimu yaliyo weka historia Duniani mwaka 2013/2014



      Madudu (5) matano  ya  Wizara ya Elimu yaliyo weka historia Duniani mwaka 2013/2014
   Mwaka 2013 na 2014  umekuwa ni mwaka wenye maajabu ya madudu ambayo hayajawahi kutokea katika sekta ya elimu Tanzania.Maajabu hayo nikama  yafuatayo
1.MATOKEO
Kutangaza matokeo ya kidato channe ya mwaka 2013/2014 kwa viwango vipya vya madaraja ya ufaulu yaliyo pingwa sana na watanzania na Wabunge bungeni  Kabla yakutumika kwa kuwa  viwango hivyo ambavyo havileti maendeleo katika sekta ya elimu zaidi ya kudhorotesha sekta ya elimu Tanzania.
2.Ajira
27/2/2014 Wizara kupitia gazeti la Tanzania Daima ilitangaza kuwa imewaajiri walimu 360000 bila kutoa majina ya walimu hao na ambao wameajiriwa kitu ambacho hakikuwahi kutokea tangu Wizara hiyo ilipoanzishwa.
3.Mazoezi ya Vitendo
Mazoezi ya vitendo kwa walimu Tarajari waliopo vyuoni haijawahi kutokea wakachelewa kwenda kwenye mazoezi hayo ya vitendo kama ilivo sasa mwezi wapili unaisha bado tu wapo vyuoni bila sababu za maana.
4.Kusoma nakuandika
 Haijawahi kusikika Duniani kote kuwa kuna wanafunzi wanaomaliza shule ya msingi na kufanya mitihani kisha kufaulukuendelea  na wanapoenda shule ya upili yaani secondari washindwe kusoma na kuandika lakini kwa Tanzania hilo lime tokea na limesha zoeleka na kuwa kama kitu cha kawaida tu.
5.Tovuti
Mwisho kabisa ukiingia kwenye tovuti yao ya wizara ya Elimu kunasehemu ya kutoa maoni ya Yule anaetazama tovuti hiyo watu wengi wamekuwa wakitoa maoni kuwa mfumo ni mbovu kwa zaidi ya  48% Kitu ambacho ni ajabu kutokea kwa nchi nyingine pia tovuti hiyo haivutii kila siku vitu nivilevile.
             INCHI YENYE UTAWALA BORA HAIWEZI KUWA NA ELIMU MBOVU

Hakuna maoni: