Jumatano, 5 Machi 2014

Ajira mpya za wlimu 2013/2014

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA AJIRA KWA WALIMU WAPYA MWAKA 2013/14

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK HAPA CHINI

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA AJIRA KWA WALIMU WAPYA MWAKA 2013/14

Jumla ya Walimu wapya 36,021 ambao wamehitimu mwaka 2013 kutoka vyuo mbalimbali hapa nchini wataajiriwa rasmi na Mamlaka za Serikali za Mitaa (Halmashauri) ifikapo tarehe 01 Aprili 2014. Kati ya idadi hiyo walimu wa ngazi ya Cheti (Daraja III A) ambao hufundisha katika shule za Msingi ni 17,928 na walimu wa shule za sekondari ni 18,093 (wakiwemo 5,416 wa Stashahada na 12,677 wenye shahada).

Orodha rasmi ya walimu wapya ikionesha Halmashauri mbalimbali walikopangwa itatangazwa kwenye tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI (www.pmoralg.go.tz) na ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (www.moe.go.tz) ifikapo tarehe 15 Machi, 2014.

Walimu wote wapya wanatakiwa kuripoti bila kukosa kwenye Halmashauri walikopangiwa ifikapo tarehe 01 Aprili, 2014 ili waanze kazi mara moja.

Inasisitizwa kwamba walimu waripoti tarehe hiyo ili taarifa zao za kiutumishi zifanyiwe kazi na Waajiri wao yaani Wakurugenzi ili kuwawezesha kupata mshahara mwezi Aprili 2014 na hivyo kuepuka ulimbikizaji wa mshahara kwa watumishi wapya wanaoanza ajira.

Mwalimu yoyote ambaye ataripoti baada ya tarehe 10 Aprili, 2014 bila sababu za msingi zinazokubalika kiutumishi atakuwa amepoteza nafasi hiyo.

Ikumbukwe kwamba Upangaji wa Walimu wapya kwenye Halmashauri umezingatia uwepo wa mahitaji ya walimu. Vile vile, fedha za kujikimu kwa muda wa siku saba na nauli ambazo zitalipwa kwa kila mwalimu atakayeripoti kulingana na viwango vilivyowekwa na Serikali zimetumwa kwenye Halmashauri walikopangwa walimu hao. Hivyo, kila mwalimu anatakiwa kwenda kuripoti katika Halmashauri alikopangwa.

Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI haitafanya mabadiliko yoyote ya vituo vya kufanya kazi walimu wapya isipokuwa kwa utaratibu wa kawaida wa uhamisho baada ya mwalimu kutimiza vigezo na masharti ya uhamisho.

Ni vema ifahamike kuwa ajira zinazotangazwa ni za walimu wapya. Walimu ambao tayari ni watumishi umma waliokuwa vyuoni kwa ajili ya kujiendeleza kielimu na hivi sasa wamehitimu mafunzo yao, wanatakiwa kurudi kwa waajiri wao na kuendelea na kazi.

IMETOLEWA NA
JUMANNE A. SAGINI
KATIBU MKUU
OFISI YA WAZIRI MKUU - TAMISEMI

Jumatatu, 3 Machi 2014

WIZARA YA ELIMU ELIMU TANZANIA YAZIDI KUBORONGA



                                                   
    Wizara ya elimu ya Tanzania imeendelea kufanya hovyo katika maamuzi na utendaji wa           mambo   yake.
 Halii hii inajidhihirisha kwa kuwapa walimu tarajali (walimu waliopo vyuo vya Serikali,wa ngazi ya cheti na Stashahada) pesa  ya kujikimu  wakiwa  katika mazoezi ya vitendo  (field) kiasi cha  shilingi  4500 (elfu mianne na miatano tu ) .
Hii sio bahati mbaya kwa sababu utaratibu huo wakuwapa wanavyuo hao wanaosomea ualimu ulianza mwaka jana na walilipwa pia 4500 wakiwaahidi kuwa kwa  kuwa ni mfumo mpya hivyo mwaka utakaofuatia yaani mwaka huu wa 2014 wange waongeza pesa lakini hali imebakia kuwa hivyo hivyo.

Utaratimu wa miaka yanyuma 2012 kurudi nyuma ilikuwa wanachuo walio katika vyuo vya ualimu vya serikali  wanapoenda kwenye mazoezi ya vitendo walikuwa wakipewa chakula na fedha kiasi za kujikimu wanapo kuwa huko lakini kwanzia mwaka jana wamekuwa wakipewa shilingi 4500 tu.
 Katika hali ya kawaida tujiulize hiyo pesa inatosha nini ikiwa wanavyuo waliopo vyuo vikuu huwa wanalipwa shilingi 7500 kwa siku kama pesa yao ya kula wakiwa chuoni na wanapo enda (field) kwenye mazoezi ya vitendo huwa walipwa (10000) elfu kumi .

 Ukiangalia mazingira ya hawa walimu wavyuo vikuu na wa stashahada hata Cheti  wote wanaenda Field maeneo yale yale na maanisha shule zile zile na kama changamoto ni sawa tu sasa kwanini kuwe na tofauti  za posho za kujikimu wanapo kuwa huko huu ni udhaifu wa hali ya juu Wizara inabidi iji sahihishe katika upangaji wake wa mambo.Na hiyo pesa ya shilingi 4500 haitoshi kwa maisha ya sasa mtasababisha wadogo zetu wakike kujiuza huko na kuvunja ndoa za watu.
Kama haiwezekani utaratibu wa zamani ukirudishwa ni vizuri pia.

Maana ikiwa watu wanagomea laki tatu Bungeni kwenye Bunge La katitiba  hawa wanaokubali 4500 unadhani vichwani mwao wafikiria nini  kama sio ni mgomo baridi?.
   
Nchi yenye utawala Bora haiwezi kuwandaa Bora walimu na sio Walimu Bora.
                              Wakikuuliza kaandaa nani waambie korumba Mtanzania