Wizara ya elimu ya Tanzania imeendelea kufanya
hovyo katika maamuzi na utendaji wa mambo yake.
Halii hii inajidhihirisha kwa kuwapa walimu
tarajali (walimu waliopo vyuo vya Serikali,wa ngazi ya cheti na Stashahada)
pesa ya kujikimu wakiwa
katika mazoezi ya vitendo (field)
kiasi cha shilingi 4500 (elfu mianne na miatano tu ) .
Hii sio bahati mbaya
kwa sababu utaratibu huo wakuwapa wanavyuo hao wanaosomea ualimu ulianza mwaka
jana na walilipwa pia 4500 wakiwaahidi kuwa kwa
kuwa ni mfumo mpya hivyo mwaka utakaofuatia yaani mwaka huu wa 2014
wange waongeza pesa lakini hali imebakia kuwa hivyo hivyo.
Utaratimu wa miaka
yanyuma 2012 kurudi nyuma ilikuwa wanachuo walio katika vyuo vya ualimu vya
serikali wanapoenda kwenye mazoezi ya
vitendo walikuwa wakipewa chakula na fedha kiasi za kujikimu wanapo kuwa huko
lakini kwanzia mwaka jana wamekuwa wakipewa shilingi 4500 tu.
Katika hali ya kawaida tujiulize hiyo pesa
inatosha nini ikiwa wanavyuo waliopo vyuo vikuu huwa wanalipwa shilingi 7500
kwa siku kama pesa yao ya kula wakiwa chuoni na wanapo enda (field) kwenye
mazoezi ya vitendo huwa walipwa (10000) elfu kumi .
Ukiangalia mazingira ya hawa walimu wavyuo
vikuu na wa stashahada hata Cheti wote
wanaenda Field maeneo yale yale na maanisha shule zile zile na kama changamoto
ni sawa tu sasa kwanini kuwe na tofauti
za posho za kujikimu wanapo kuwa huko huu ni udhaifu wa hali ya juu
Wizara inabidi iji sahihishe katika upangaji wake wa mambo.Na hiyo pesa ya
shilingi 4500 haitoshi kwa maisha ya sasa mtasababisha wadogo zetu wakike
kujiuza huko na kuvunja ndoa za watu.
Kama haiwezekani
utaratibu wa zamani ukirudishwa ni vizuri pia.
Maana ikiwa watu wanagomea laki tatu Bungeni kwenye Bunge La katitiba hawa wanaokubali 4500 unadhani vichwani mwao wafikiria nini kama sio ni mgomo baridi?.
Nchi yenye utawala Bora haiwezi kuwandaa Bora
walimu na sio Walimu Bora.
Wakikuuliza kaandaa nani waambie korumba Mtanzania
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni