CHADEMA NDANI YA UDOM.
Sisi wanaharakati tulioko Udom,kesho tutafanya mkutano pale nje kidogo
ya kitivo cha Elimu, lengo ni kuwaelimisha vijana wenye mawazo ya
ki-CCM, hapo tutaonesha jinsi chadema ilivyo imara na ilivyo na uwezo wa
kuchukua maamuzi magumu ndani ya chama kwa maslahi ya taifa kitu
ambacho ccm hawawezi kwani walisha shindwa, mfano ni pale CCM
iliposhindwa kuwavua gamba magamba wao kwa sababu ndani ya ccm hakuna
msafi awezaye kumnyooshea mwenzake kidole-wote ni mafisadi
tofauti na CHADEMA ambayo kila mmoja ni msafi kwa nafasi yake na
akijitokeza msaliti,dhaifu, na fisadi anaondolewa haraka na kimbilio huo
ni CCM kwani ndicho kichaka cha waovu,chadema hatuna nafasi ya
waovu.nitumie nafasi hii kuwaalika kwenye mkutano huo wa kesho jumamosi
pale UDOM kwenye ofisi zetu, mliopo udom na nje ya UDOM tunaomba mtuunge
mkono, muda si mrefu tutaanza kutoa elimu kuhusu katiba ya chadema na
nchi kupitia blog yetu ambayo ntaitangaza kupitia mitandao mbalimbali ya
kijamii ikiwemo kundi hili, lengo ni kuwaelimisha watanzania kuongea
kwa kutumia mareje ya vifungu vya sheria kwa sababu haki hapelekewi mtu
bali huidai mwenyewe.kwa maana hii basi bila kuifahamu sheria inayokupa
haki fulani huwezi kuidai haki, hii ndo nafasi ambayo mafisadi
wanaitumia kutunyang'anya haki yetu watanzania. Watanzania simameni
tudai haki zetu, na CHADEMA ndilo jiko la walio bobea sheria, ukiwa
mwana-chadema tayari wewe ni mwanasheria kwa maana moja ya jukumu letu
ni kuielimisha jamii kuhusu utawala wa kisheria. Mungu ibariki
Tanzania,Mungu ibariki CHADEMA, Mungu ibariki CHADEMA tawi la UDOM.
Katibu wa CDM-Tawi la UDOM. Marigiri.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni